Bi
Razia Mwawanga kutoka IAWRT akifungua mkutano wakati wa uzinduzi wa
ripoti ya utafiti kuhusu wanawake wanavyopewa nafasi hasa katika vyombo
vya habari hasa hapa nchini.
Mkurugenzi
wa Shirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of
Women in Radio and Television (IAWRT) Tanzania Bi. Rose Haji Mwalimu
akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti kuhusu
wanawake wanavyopewa nafasi hasa katika vyombo vya habari hasa hapa
nchini.
Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa TAMWA, Bi. Edda Sanga (kushoto) akiwahamasisha
wanawake kuwa na uthubutu ili kuyafikia malengo waliyojiwekea na
kutojiona hawawezi kisa wao ni watoto wa kike, kulia ni Mkurugenzi wa
IAWRT Tanzania Bi. Rose Haji Mwalimu.
Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa TAMWA, Bi. Edda Sanga(kushoto) pamoja na Mkurugenzi
washirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of
Women in Radio and Television (IAWRT) Tanzania Bi. Rose Haji Mwalimu
wakizindua ripoti ya utafiti kuhusu mwanamke au mtoto wa kike anavyopewa
nafasi hasa kwenye vyombo vya habari.
Wajumbe wa IAWRT wakiangalia moja ya filamu inayohusu nafasi ya mwanamke hasa katika jamii.
Wajumbe wa mkutano huo wakiendelea kutoa maoni yao kuhusu usawa wa kijinsia katika ngazi mbalimbali za maamuzi.
Picha ya pamoja.
Na Mwandishi wetu
Katika
ripoti iliyotelewa awali na Shirika lisilo la kiserikali nchini la
International Association of Women in Radio and Television Tanzania
(IAWRT), imeonyesha kwamba wanawake au mtoto wa kike hapewi nafasi ya
moja kwa moja katika kutoa taarifa au katika shughuli za kufanya maamuzi
katika ngazi mbali mbali tofauti na watoto wa kiume au mwanaume.
Utafiti huo umebaini kwamba mbali na kutopewa mtoto wa kike nafasi ya
kufanya maamuzi katika ngazi tofauti, ambapo wamesema inapelekea wanaume
kupata kipato kikubwa zaidi ya wanawake.
Katika
hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi wa TAMWA, Bi. Edda Sanga,
ambapo ameiomba serikali na vyombo vya habari kuwapa kipaumbele wanawake
katika ngazi tofauti tofauti za uongozi ili kuweza kuondoa lile tabaka
lililopo kati ya mwanamke na mwanaume, na pia inaweza kuchangia katika
maendeleo na mabadiliko ya nchi kiujumla. Aliongezea kwa kusisitizia
kuwa wanawake wenyewe washirikiane na wajitume pale wanapopata fursa
katika matukio, na pale wanapofanikiwa warudi kuja kusaidia kuinua
wanawake wengine ambao bado hawajaweza kufika pale panapohitajika.
Akizungumza
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali nchini la International
Association of Women in Radio and Television (IAWRT) Tanzania, Bi. Rose
Haji Mwalimu alisema kwa wanawake inabidi wajitambue na pia wajue
thamani zao katika jamii ili waweze kufikia malengo yao. Hayo aliyasema
wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti kuhusu Mwanamke au mtoto wa kike
anavyopewa nafasi hasa kwenye vyombo vya habari ambapo ilionekana mtoto
wa kike hapewi nafasi sawa na mtoto wa kiume.
Hii
imekuwa ni changamoto hasa kwa nchi za Afrika kutomthamini mtoto wa
kike. Pia lisisitiza kuwa licha ya juhudi nyingi za wanahabari na
taasisi za habari kuwainua wanawake na wasichana katika vyombo vya
habari mathalani Radio bado juhudi zinakabiliana na changamoto kadhaa
licha ya kuzaa matunda kwa sehemu ndogo na kupelekea mwanaume kuwa na
nafasi kubwa katika vyombo hivyo.
No comments:
Post a Comment