Afisa
Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za
Kulevya na Uhalifu (UNODC), Immaculata Nyoni akizungumza jambo kabla ya
kukabidhi vifaa vya maabara kwa Jeshi la Magereza nchini.
Kamishna
wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akizungumza
jambo wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa vya maabara kwa
Magereza Tanzania.
Afisa
Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za
Kulevya na Uhalifu (UNODC), Immaculata Nyoni pamoja na Kamishna wa
Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa wakikata utepe
kuashiria kukabidhiwa vifaa vya maabara vilivyotolewa na Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC).
Afisa
Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za
Kulevya na Uhalifu (UNODC), Immaculata Nyoni akitolea ufafanuzi vifaa
vya maabara alivyokabodhi kwa Jeshi la Magereza ili kusaidia kuwapima
wafungwa walioko magerezani.
Kamishna
wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akitoa
shukrani baada ya kupokea msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) lililowakilishwa
na Immaculata Nyoni.
Hivi ndivyo vifaa vya maabara vilivyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza.
Picha ya pamoja.
Na Mwandishi wetu
Jeshi
la Magereza Ukonga limepokea vifaa vya maabala kutoka Shirika la Umoja
wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC)
ambavyo vitasaidia kutoa vipimo kwa wafungwa waliofungwa magerezani hii
ikiwa ni jitihada za kupunguza matumizi ya dawa za kulevya katika
magereza hapa nchini.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo Bi. Immaculata Nyoni ambaye ni Afisa
Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za
Kulevya na Uhalifu (UNODC) alisema wametoa msaada huo baada ya kufanyika
kwa tafiti hasa kwenye magereza hapa nchini na utafiti huo Magereza
ilishirikiana na UNODC na kubaini changamoto wanazozipata wafungwa
wakati wa kupimwa afya zao.
Hivyo
kama shirika limeamua kutoa msaada wa vifaa vya maabala ambavyo ni
Hematology mbili(2), Urine Analyzer tatu (3) pamoja na Hemoglobin
Mashine mbili(2) na vifaa hivi vimegharimu takribani shilingi milioni 10
za kitanzania. Akitoa shukrani Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa
Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa kwa niaba ya Mkuu wa Magereza hapa
nchini amesema anawashukuru UNODC kwa kuona matatizo yanayowakabili hasa
kwenye hospitali za Magereza zinazohudumia wafungwa na kuamua kutoa
msaada huo kwa jeshi hilo.
Pia
alisisitizaushirikiano kati ya Jeshi la Magereza pamoja na Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC)
kuimarishwa ili kuweka ukaribu kwa kila jambo linalohusu afya ya
wafungwa hasa kwa wale waliokuwa wanatumia madawa ya kulevya na wenye
virusi vya UKIMWI.
Baada
ya wauguzi kupokea msaada huo walisema sasa ni muda wa kazi tu kwani
wamepata vifaa ambavyo vitaweza kuwahudumia wagonjwa kwa wakati kwani
hapo mwanzo kulikuwa na uhaba wa vifaa vya maabara na kupelekea matibabu
kutokuwa ya uhakika katika hospitali za Magereza zinazohudumia
wafungwa.
No comments:
Post a Comment