Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahidi kumshughulikia
Bungeni, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kikidai
kuwa bado hajasafishwa kwenye kashfa ya akaunti ya Escrow.
Ahadi hiyo ilitolewa juzi na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, John
Mnyika katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo
la Handeni, akimnadi Daudi Lusewa.
Alisema baadhi ya mawaziri, akiwamo Muhongo, bado hawajasafishwa na
tuhuma za rushwa zilizosababisha wajiuzulu hivyo wajiandae kwani wabunge
wa chama hicho wamejiandaa kumwangusha.
Mnyika alisema amemshangaa kuona Rais John Magufuli akimteua Muhongo
kwenye Wizara ile ile alikopatia kashfa, iliyosababisha Rais mstaafu
Jakaya Kikwete kumtema kwenye Baraza la Mawaziri.
“Hatukubaliani na uteuzi wa Profesa Muhongo na namhakikishia bungeni
patachimbika,” alisema Mnyika ambaye ni Mbunge wa Kibamba, Dar es
salaam.
“Hoja yetu ya kwanza tutakapoingia bungeni tu itakuwa kushinikiza Waziri huyu ajiuzulu maana bado hajasafishwa,” alisema Mnyika.
No comments:
Post a Comment