Waziri
wa Maji na Umwagiliaji nchini Tanzania Profesa Makame Mbarawa
ameliagiza Shirika la Maji Safi na Maji Taka Jijini Dar es Salaam
(DAWASCO) kuona namna ya kuweka mita za maji ambazo mteja hatoweza
kutumia maji iwapo hajalipia kwanza (Prepaid).
Akizungumza
leo Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza
katika shirika hilo, Profesa Mbarawa amesema kwa kuwekwa kwa mita hizo
kutaisaidia kuiongezea serikali mapato na kuwadhibiti wateja wasiolipa
ankara za maji kwa wakati.
Prof
Mbarawa ameongeza kuwa mita hizo mpya zitawawezesha Wananchi kutumia
maji kwa kadri kiasi anachotumia ili kuepusha malalamiko ya kuongezewa
bili lakini pia kuepusha utumiaji wa maji bila kulipia.
Profesa
Mbarawa pia ameliagiza kampuni ya maji safi na taka DAWASCO kuhakikisha
inaweka miundo mbinu ya kisasa ambayo itawezesha maji taka kupita bila
ya kumwagika ili kuzuia uchafuzi wa mazingira.
No comments:
Post a Comment