KAMATI
Maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein imewataka
wananchi na wanachama kujiweka tayari na hatimaye kujitokeza katika
uchaguzi mkuu wa marudio.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride
Bakari Jabu, wananchi wametakiwa kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio na
kuachana na propaganda zinazotolewa na watu wachache kwa lengo la
kupotosha ukweli.
“Kikao
cha Kamati Maalumu ya CCM Zanzibar kilichokutana hapa chini ya
Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar, Dk Shein kimewataka wananchi,
wanachama na wafuasi wa CCM kujitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa marudio
ambao tarehe ya kufanyika kwake itatangazwa na taasisi husika,” imesema taarifa hiyo ya Waride.
Matokeo
ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25 ulifutwa na Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha kwa kile
alichoeleza ni kuwepo kwa ukiukwaji wa kanuni na sheria za uchaguzi huru
wa kidemokrasia.
Katika
kikao cha jana kilichohudhuria pia na viongozi kadhaa wa kitaifa
akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu
Hassan, kilijadili ajenda mbili ikiwemo hali ya kisiasa mara baada ya
uchaguzi mkuu kwa upande wa CCM.
Katika
taarifa hiyo, chama hicho kimesema kimeridhishwa na mwenendo wa hali ya
kisiasa na kimewapongeza wanachama waliojitokeza kwa wingi kushiriki
katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Aidha
chama kimepongeza na kutoa baraka kwa mazungumzo yanayoendelea ya
viongozi wakuu wa kisiasa yakiwa na lengo la kuleta amani ya kudumu.
Kamati ya mazungumzo ya hali ya kisiasa Zanzibar yenye lengo la kusaka
amani ya kudumu iliyovurugika kutokana na kufutwa kwa uchaguzi mkuu
inaundwa na viongozi wastaafu wakiwemo marais, Dk Salmin Amour, Amani
Abeid Karume, Balozi Seif Ali Iddi ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Sharif Hamad na Rais
wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.
Akizungumza
juzi Ikulu, jijini Dar es Salaam, Rais wa Zanzibar, Dk Shein alisema
mazungumzo hayo yanaendelea vizuri na taarifa kamili yatakapofikia
tamati. Alipoulizwa kuhusu hatma ya CCM kama uchaguzi mkuu utarudiwa,
Waride alisema chama bado kiko imara na hakijatetereka.
No comments:
Post a Comment