Afisa
wa Polisi Mkoani Arusha aliyetajwa kama PC Halfani, alikutwa akiwa
amejinyonga katika eneo la kambi ya makazi ya askari wa jeshi la polisi
jijini humo jumapili iliyopita.
Askari
huyo ambaye alikuwa anahusika na ulinzi wa kutumia polisi na farasi
alikutwa na wakazi wa eneo hilo akiwa amening’ing’inia juu ya mti huku
sababu za kujitoa roho kwa hali ya kusikitisha zikiwa kitendawili.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa ARusha, Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo japo alikataa kutoa maelezo kuhusu tukio hilo akidai kuwa
hilo ni tukio lisilopaswa kutolewa maelezo kwa umma.
“Mambo yanayohusiana na polisi hayapaswi kwenda kwenye vyombo vya habari,” alisema Liberatus Sabas.
Wakazi
wa eneo hilo la makazi ya polisi walitoa heshima zao za mwisho kwa
mwili wa marehemu kabla haujasafirishwa kwenda mkoani Singida kwa ajili
ya mazishi.
No comments:
Post a Comment