Mshiriki
wa mafunzo ya Airtel Fursa mkoani Iringa Bi Fatuma Mkini (kushoto )
akipokea cheti cha ushiriki wa mafonzo hayo kutoka kwa afisa mahusiano
na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki mara baada ya mafunzo ya Airtel
Fursa kumalizika mkoani Iringa kwa vijana zaidi ya 200 kushiriki.
Vijana
washiriki wa mafunzo ya siku moja ya Airtel Fursa mkoani Iringa
wakimsikiliza afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki
(kulia) wakati wa ufungizi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi
wa Highland mjini Iringa jana.
wawakilishi
wa vijana zaidi ya 200 mkoani Iringa walioshiriki kupata mafunzo ya
ujasiriamali kupitia mradi wa Airtel fursa wakiwa katika picha ya pamoja
na afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki na wafanyakazi
wengine wa Airtel mkoa wa Iringa mara baada ya kukabidhiwa vyeti kwa
niaba ya wenzao.
Baada ya
kukata tamaa ya maisha kwa muda mrefu baadhi ya vijana mkoani Iringa
wameeleza kufurahishwa na kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kwa
kuwapatia mafunzo ya jinsi ya kuanzisha na kuendesha biashara zao kwa
faida kupitia mpango wa Airtel FURSA.
Wakizungumza
na mara baada ya mafunzo ya siku moja ya Airtel FURSA yaliyofanyika
katika ukumbi wa Highlands mjini Iringa kwa kuwashirikisha vijana zaidi
ya 200,washiriki hao walisema kuwa mafunzo hayo ni ukomb0zi mkubwa kwao
kwani baadhi yao walikuwa wakilazimika kushinda vijiweni kutokana na
kukosa fursa ya mafunzo kama hayo .
Washiriki
wa mafunzo hayo Bi Husna Sanga na Bw Okelo Kasim wakizungumza kwa niaba
ya wenzao walisema kuwa mbali ya kuwa wa hatua ya kampuni hiyo ya simu
ya Airtel kutoa mafunzo hayo si tu kunawasaidia kupata elimu kuendesha
biashara na miradi mingine ya kiuchumi bali ni sehemu ya ukombozi kwao
na familia zinazowazunguka .
Alisema
Bi Sanga kuwa sehemu kubwa ya vijana hasa mabinti walikuwa wakirubunika
na kujiingiza katika biashara zisizofaa kama za uuzaji wa miili yao
kutokana na kutokuwa na elimu ya uanzishaji wa biashara ndogo ndogo
ambao zingewakomboa kiuchumi hivyo kupitia mpango huo wa Airtel FURSA ni
wazi kilio chao kimepata majibu.
“Wapo
baadhi ya mabinti wenzetu ambao wanalazimika kufanya biashara ya kuuza
miili yao ili kupata kipato na mwisho wa siku wanapoteza maisha kwa
ugonjwa wa UKIMWI , ila kwa sisi ambao tumepata elimu hii kupitia Airtel
FURSA tunaweza kuwa mfano kwa wengine ambao wanafikiri kazi ni kuuza
miili yao pekee”
Huku Bw
Kasim mbali ya kupongeza kampuni ya simu ya Airtel Tanzani kwa
kuwakumbuka vijana bado alisema kuwa kama njia ya wao kupongeza kampuni
hiyo ya simu kwa vijana wote waliopata mafunzo hayo kwenda kuonyesha
mfano kwa wenzao kwa kufanya kazi ya kubuni miradi na kuendesha shughuli
zao kifanisi zaidi.
Kwa
upande wake afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki kuwa
Kutokana na mradi huo wa Airtel FURSA vijana wengi watanufaika zaidi na
wanafaidika na mradi huo ni wale wenye miaka kati ya 18-24
Alisema
kuwa mradi huo umelenga kuwafikia vijana kote nchini na hadi sasa zaidi
ya mikoa tisa wamefikiwa na mradi huo wa Airtel FURSA .
Bi Kaniki
alitaja mikoa ambayo tayari imefikiwa na mradi huo Mbeya, Arusha,
Dodoma, Mtwara, Mwanza, Mtwara, Dar es Salaam , morogoro, Tanga, Tabora
na Iringa kuwa hadi sasa zaidi ya vijana 1700 wamefikiwa.
Alisema
kuna njia mbili za kuwawezesha vijana njia ya kwanza kupatiwa Mafunzo ya
ujasiriamali na njia ya pili kupatiwa vitendea Kazi .
Hivyo
aliwataka vijana wote nchini ambao watasikia taarifa ya kuwepo kwa
Airtel Fursa katika Mkoa wao basi kuweza kuchangamkia Fursa hiyo ambao
hutolewa bure.
Alisema
ili kijana aweze kufaidika au kushiriki kwenye Airtel FURSA atatakiwa
kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:-
Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao
kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara.
Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com
Alisema
kuwa Airtel Fursa inawalenga vijana ambao wapo katika biashara na wale
ambao hawana shughuli na wanataka kuanzisha shughuli pia kwao ni fursa
kwao .
Aidha
alisema kuwa tayari baadhi ya vijana wamepata kunufaika na mradi huo
ambao umelenga kuwainua vijana na kuongeza kuwa mradi huo ulioanza mwaka
huu utakuwa ni mradi endelevu.
No comments:
Post a Comment