Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa kwanza
kulia) akizungumza na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mara baada ya kuwasili katika kituo
cha kuzalisha umeme wa maji cha Mtera ili kukagua kituo hicho na
kuzungumza na wataalam.Wa Tatu kulia ni Kamishna wa Nishati na Maendeleo
ya Petroli, Mhandisi Hosea Mbise), na wa Nne kulia ni Mkurugenzi wa
Idara ya Sheria Wizara ya Nishati na Madini, Justus Mulokozi.
Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (katikati)
akikagua kituo cha kuzalisha umeme wa maji cha Mtera mara baada ya
kufanya mazungumzo na watendaji wa Tanesco wanaosimamia kituo hicho. Wa
Kwanza Kushoto ni Kaimu Meneja wa Kituo cha Mtera, Eng. Manfred Mbyallu
na kulia ni Meneja Uzalishaji Umeme wa Maji nchini, Antony Mbushi.
Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa kwanza
kushoto waliokaa) akiwa katika chumba cha kuongozea mitambo ya
uzalishaji umeme katika kituo cha kuzalisha umeme cha Kidatu mkoani
Morogoro wakati alipofanya ziara katika kituo hicho. Katikati (waliokaa)
ni Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Hosea Mbise
na Wa Kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Sheria Wizara ya Nishati na Madini,
Justus Mulokozi.
Muonekano
wa Bwawa la Mtera kwa sasa, baada ya maji katika bwawa hilo kupungua
kwa kiasi ambacho hakiruhsu umeme kuendelea kuzalishwa na kupelekea
mitambo ya umeme kuzimwa tarehe 7 Oktoba, 2015.
Katibu
Mkuu,Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi Omar Chambo (wa tatu kulia)
akiangalia kiasi cha maji kilichopo katika Bwawa la Kidatu mkoani
Morogoro ambapo kimepungua kutoka mita 450.00 hadi mita 439.48 kufikia
tarehe 27 Novemba 2015.Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Nishati na
Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Hosea Mbise.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini (aliyevaa suti) akisikiliza maelezo
kuhusu uzalishaji wa umeme katika bwawa la Kidatu mkoani Morogoro,
wakati alipofanya ziara katika bwawa hilo. Anayetoa maelezo ni Meneja wa
Kituo cha Kidatu, Eng. Justus Mtolera.
Kaimu
Meneja Mwandamizi Uzalishaji Umeme wa Maji nchini, Lewanga Tesha
(aliyesimama) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
Madini, Mhandisi Omar Chambo (katikati) kuhusu uzalishaji umeme wa maji
nchini katika ziara ya Katibu Mkuu kwenye vituo vya Kidatu na Mtera.Wa
kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa Kituo cha Mtera, Eng. Manfred Mbyallu.
Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa kwanza
kushoto) akipata maelezo kuhusu kipimo kinachoonyesha kima cha maji
katika bwawa la kuzalisha umeme la Mtera. Bwawa hilo lilisimamisha
uzalishaji tarehe 7 Oktoba 2015 kutokana na kima cha maji kuwa chini ya
kiasi kinachoruhusiwa kuzalisha umeme.Anayetoa maelezo ni Kaimu Meneja
wa Kituo cha Mtera, Eng. Manfred Mbyallu (wa pili kutoka kulia).
No comments:
Post a Comment