Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Bw. Ban Ki Moon pichani. Ametuma salamu
za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.
[IKULU]
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari mapema leo na
Ikulu, Imeeleza kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Bw. Ban Ki
Moon ametuma salamu hizo za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambaye tayari
ameanza kazi kwa kishindo tokea kuapishwa kwake hiyo Novemba 5, mwaka
huu kuwa Rais wa Tanzania.
“Uchaguzi
wa mwaka 2015 ni uthibitisho wa wazi na dhamira ya muda mrefu ya
Watanzania kwa demokrasia, amani na utulivu. Nina imani kuwa masuala ya
uchaguzi yaliyobakia yatashughulikiwa kupitia taratibu za kisheria
zilizopo kwa njia ya amani na uwazi.” Bw. Ban Ki Moon amesema kwenye barua yake ya pongezi ambayo amemtumia Mhe. Rais Dkt. Magufuli.
Bw.
Ban Ki Moon amesema anaamini kuwa, chini ya uongozi wa Dkt. Magufuli,
Serikali ya Tanzania itashughulika na juhudi za kuondoa umaskini,
kuimarisha utawala bora na kuendeleza juhudi za Tanzania katika
kupigania amani na utulivu katika Ukanda wa Afrika Mashariki na nje
zaidi ya Ukanda huu.
“Napenda kukuhakishia kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kukuunga mkono pamoja na Serikali yako katika juhudi hizi”. Mhe. Ban Ki Moon amesema.
Katibu
Mkuu Bw. Ban Ki Moon pia ameipongeza Tanzania kwa kuwa mwenza imara na
wa kutumainiwa na Umoja wa Mataifa kwa miongo yote.
“Nathamini
ushirikiano uliopo baina ya Umoja wa Mataifa na nchi yako na katika
kuendeleza malengo ya UN, nakutakia mafanikio katika kutekeleza shughuli
zako”. Bw. Ban Ki Moon amesema katika salamu zake.
No comments:
Post a Comment