Mkazi
wa eneo la Duluti wilayani Arumeru mkoani Arusha,Janet Tinai
akilalamika mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) akiwa na
baadhi ya vyombo vyake mara baada ya kuhamishwa kwa amri ya mahakama na
kampuni ya Majembe Auction Mart juzi.
[ARUMERU] Serikali imeombwa
kuingilia kati sakata la familia ya Juma Isangu mkazi wa eneo la Duluti
wilayani Arumeru mkoani Arusha kuondolewa na kisha kuvunjiwa nyumba
waliyokuwa wakiishi kwa amri ya mahakama kwa madai haki haikutendeka.
Familia hiyo iliondolewa
juzi majira ya saa 6;30 juzi mchana na kampuni ya udalali wa mahakama
ya Majembe Auction Mart Ltd tawi la Arusha kwa madai kwamba waliagizwa
na msimamizi wa mirathi wa nyumba hiyo aitwaye,Janeth Fosbrooke
kuwaondoa kwa kuwa hawastahili kuwepo ndani yake.
Akizungumza mbele ya waandishi wa
habari waliofika katika eneo hilo, Isangu akiwa na mkewe,Janet Tinai
pamoja na mtoto wao wa kiume,Issa Juma alisema alisema kwamba kwa sasa
hawaelewi ni wapi wataishi kwa kuwa kitendo cha kuondolewa katika nyumba
hiyo na kisha kutupiwa virago hakikufuata sheria.
Alisema kwamba wameondolewa
kinyemela ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi bila taarifa ingawa hapo
awali waliwahi kushinda kesi ya mgogoro wa nyumba hiyo nambari 33 ya
mwaka 2011 iliyofunguliwa katika mahakama ya ardhi.
Akielezea tukio hilo Tinai alisema
kwamba mnamo juzi majira ya saa 6;30 mchana watu wapatao sita ambao
walijitambulisha kwamba ni madalali wa mahakama kutoka kampuni ya
Majembe Auction Mart walifika katika nyumba wanayoishi wakiambatana na
askari wa jeshi la polisi na kuwataka kutoka nje ya nyumba hiyo.
Tinai,alisema kwamba wakiwa
wanajiuliza ndipo watu hao waliingia ndani na kisha kuanza kutoa baadhi
ya mali mbalimbali na kisha kuzipeleka ndani ya lori mojawapo lililokuwa
limeegeshwa nje ya nyumba hiyo na kuacha baadhi ya vitu nje ya eneo la
nyumba hiyo.
Alisema kwamba na mara walipohoji
walijibiwa ya kwamba hawakutakiwa kuendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo
kwa kuwa kuna amri kutoka mahakama kuu inayowataka kuondoka mara moja
ndani ya nyumba hiyo .
Hatahivyo,kwa nyakati tofaiti
wanafamilia hao walisema kwamba nyumba hiyo ni halali kwa kuwa walipewa
na marehemu Henry Fosbrooke ambaye alikuwa mmiliki halali wa eneo
hilo tangu mwaka 1980 ambaye aliacha wosia waliuwasilisha mbele ya
mahakama kuu kanda ya Arusha kama moja ya vielelezo na kisha kukubaliwa.
Hatahivyo,Mwenyekiti wa kitongoji
cha Duluti,Elias Kaaya akihojiwa na waandishi wa habari katika eneo la
tukio alisema kwamba hivi karibuni baadhi ya watu ambao walijitambulisha
kwamba ni madalali wa mahakama kutoka kampuni ya Majembe Auction Mart
walifika ofisini kwao na kuwapa taarifa kuwa wataendesha zoezi la kumtoa
mpangaji aitwaye,Isangu kwenye kitongoji chake.
Huku akionyesha barua ya mnamo Novemba 11 mwaka huu yenye KUMB No,REF.NO.MAM/ARJHF/10/2015 m wenyekiti
huyo alidai kwamba watu hao waliomba uwepo wa usimamizi kutoka ofisi
yake kumtoa mkazi huyo na kudai waliwasilisha pia taarifa kwake na jeshi
la polisi wilayani Arumeru.
“Majembe Auction Mart Ltd madalali
ya baraza la ardhi na nyumba (court blockers) ukiwa msimamizi wa amani
kwenye kata yako ya Akheri tunakuomba uwepo katika zoezi la
kumhamisha/kumtoa mpangaji ndugu Juma Isangu aliyekuwa amepangishwa na
marehemu Henry Albert Fosbrooke ambapo kwa sasa msimamizi wa mirathi
aliyeteuliwa m/s Janeth Fosbrooke ndiye ametuteua kutekeleza zoezi hili
la kumtoa mpangaji kwenye nyumba”ilisema sehemu ya barua hiyo
Hatahivyo,msimamizi wa mirathi wa
nyumba hiyo,Fosbrooke hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo lakini
msimamizi wa kampuni ya Majembe Auction Mart Ltd tawi la Arusha
,Suleiman Mdoe alisema ya kwamba wao walifuata taratibu zote kabla ya
kuwahamisha wakazi hao ikiwa ni pamoja na kubandika notisi ya siku 44
kabla ya zoezi kufanyika.
Mkazi wa eneo la
Duluti wilayani Arumeru mkoani Arusha, Juma Isangu akiwa na mkewe Janet
Tinai pamoja na mwanao,Issa Juma(katikati) wakiangalia nyaraka
mbalimbali nje ya nyumba yao mara baada ya kufukuzwa na kisha kuvunjiwa
nyumba yao juzi wilayani humo na kampuni ya Majembe Auction Mart kwa
amri ya mahakama.
Juma Isangu
akiokota baadhi ya mali zake nje ya nyumba aliyokuwa akiishi baada ya
kuondolewa ndani yake na kisha kuvunjwa kwa amri ya mahakama na kampuni
ya Majembe Auction Mart
No comments:
Post a Comment