Muonekano wa jengo la Ofisi ndogo ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kinatangaza Ratiba ya Uchukuaji Fomu za kuomba
kuteuliwa kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa wana-CCM wote wenye sifa husika.
Ratiba ya mchakato huo ni kama ifuatavyo;-
Wana-CCM
wasio Wabunge wanaoomba ridhaa ya CCM kugombea Uspika wanatakiwa
kuchukua fomu kuanzia Novemba 11, 2015 saa Sita Kamili mchana katika
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam na
kuzirejesha Novemba 12, 2015 kabla ya saa Kumi Kamili Jioni.
- Kwa wana-CCM ambao ni Wabunge wateule wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaoomba kuteuliwa kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge hilo, wanatakiwa kuchukua fomu kuanzia Novemba 11, 2015 saa Sita Kamili mchana katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam na kuzirejesha Novemba 14, 2015 kabla saa Kumi Kamili Jioni.
Fomu hizo zitatolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib.
Imetolewa na:-
KITENGO CHA MAWASILIANO NA UMMA
IDARA YA ITIKADI NA UENEZ
No comments:
Post a Comment