[Dar
es Salaam] Kampuni ya simu ya Tigo imeomba radhi wateja wake kutokana
na kukatika kwa huduma zake katika sehemu nyingine nchini jana Novemba
8.2015.
Taarifa
ya kampuni hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es
Salaam imesema kukatika kwa huduma za Tigo “kulitokana na sababu zilizo
nje ya uwezo kwa kampuni zilizo tokana na kukatika kwa mkongo sehemu
tofauti tofauti.” Aidha taarifa hiyo iliendelea kusema kwamba “tatizo
hilo sasa limeshughulikiwa kikamilifu na huduma zote za Tigo zimerejea
katika hali yake ya kawaida.’’
“Tuna
sikitishwa na usumbufu uliojitokeza kutokana na kukatika kwa huduma
zetu natunapenda kuwahakikishia wateja wetu dhamira ya kampuni yetu
kuendelea kuwapa wateja huduma zenye ubora wa hali ya juu, za kutegemewa
na kwa gharama nafuu,” amesema Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez.
Aidha
Gutierrez ametoa shukrani kwa wateja wa Tigo kwa uvumilivu wao na
kutangaza kwamba kama ishara ya kuomba msamaha kampuni ina wapa wateja
wake wote dakika 10 za muda wa maongezi, SMS za bure kwenda mtandao yote
na 10mb za kuperuzi Intaneti kwa siku nzima ya leo.Kifurushi hiki mteja
ana kipata kwa kutuma neno BURE kwenda namba 15304.
Fahamu zaidi kuhusu Tigo:
Tigo
ni kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi yenye ubunifu mkubwa
nchini Tanzania , ikijulikana kama “nembo ya maisha ya kidijitale
yanayojitosheleza”. Inatoa huduma mbalimbali kuanzia huduma ya sauti,
ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha za kwenye
mitandao ya simu za mikononi, Tigo imeanzisha ubunifu kama vile Facebook
ya Kiswahili, Kiunga cha Tigo Pesa kwa watumiaji wa simu za Android
& iOS, Tigo Music( Deezer)na huduma ya kwanza Afrika Mashariki
kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa
kubadili sarafu ya nchi husika.
Intaneti ya Tigo ya 3G inatoa huduma bora kwa wateja wake katika mikoa yote nchi nzima, na hivi karibuni tumezindua mtandao wa 4G ambao kwa sasa unapatikana Dar es Salaam nzima,na tunatarajia kuzindua nchi nzima.
Kati ya mwaka 2013 na mwaka 2014 pekee kampuni ilizindua zaidi ya maeneo
mapya 500 yenye mtandao wa Tigo na kufanya kuwa zaidi ya maeneo 2000 ya
mtandao na inapanga kuongeza uwekezaji wake mara mbili ifikapo 2017
katika suala la upatikanaji wa mtandao na kuongeza uwezo wa upatikanaji
wa mtandao kwa maeneo yasiyofikika kabisa vijijini.
Pamoja na kuwa na zaidi ya wateja milioni 9 waliosajiliwa, Tigo imeajiri
zaidi ya watanzania 300,000 ikiwa ni pamoja na mtandao wa wawakilishi
wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha za kwenye simu za
mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.
Tigo
ni nembo kubwa ya kibiashara ya kampuni la Millicom, kampuni ya
kimataifa inayoendeleza maisha ya kidijitale katika nchi 11 pamoja na
shughuli za kibiashara katika Afrika na amerika ya Kusini na ina ofisi
kubwa Ulaya na Marekani.
Pamoja na ujuzi Fulani walionao ambao unawafanya kubuni mara kwa mara na
kuwafanya wawe juu, Millicom anaendelea kujenga thamani kubwa kwa mbia;
kutumia dhana yao ya “mahitaji zaidi” hivi ndivyo wanafanya biashara
na kurejesha nafasi yao kama viongozi wa maisha ya kidijitale hasa
katika masoko zaidi ya kipekee na yenye changamoto.
Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz
No comments:
Post a Comment