Maonyesho ya 27 ya Kimataifa ya Utalii ambayo yamedumu kwa siku tatu mfululizo katika jiji la Montreal nchini Canada yafana
sana. Ubalozi wa Tanzania, Ottawa nchini Canada ulikuwa ni mmoja wa
washiriki kati ya washiriki waonyeshaji 400 walioalikwa na sekta ya
utalii ambayo ndiyo muandaaji rasmi wa maonesho hayo.
Maonyesho
hayo ambayo yamefanyika katika mahali maarufu la “la Place
Bonaventure” katika jiji la hilo, ambalo liko upande wa Mashariki mwa
Canada, eneo ambalo wengi wa wakazi wake huzungumza Kifaransa, yamekuwa
na hamasa na mashiko makubwa mwaka huu kwa kupata wahudhuriaji zaidi ya
elfu thelathini na tatu (33,000).
Kutokana
na wingi wa watu, wakiwemo watalii wanaopenda kuzuru nchi mbalimbali,
waliohamasika kuhudhuria maonesho hayo, Balozi wa Tanzania Mhe. Jack
Mugendi Zoka aliamua kuwa kati ya waonyeshaji na watoa taarifa za
vivutio vya utalii katika banda lake kama ionekanavyo katika picha hapo
chini.
Aidha,
mabalozi wa nchi mbalimbali walifika katika banda la utalii la Tanzania
kujionea ni jinsi gani limeweza kuwa kivutio cha watalii wengi. Balozi
wa nchi jirani ya Kenya alikuwa miongoni mwa watembeleaji katika banda
hilo.
Kati
ya mambo yaliyoonyesha kuwavutia watalii hao na hatimaye kutoa ahadi ya
kutembelea Tanzania ni: Mlima mrefu kuliko yote Afrika, Kilimanjaro,
ambao sasa wamefahamu uko Tanzania, mbuga za wanyama na kisiwa
kinachonukia marashi ya karafuu cha Zanzibari.
Kutoka
Tanzania Wizara ya Maliasili na Utalii iliwakilishwa na Mamlaka ya
Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ambao walikuwa sambamba za Kampuni
Binafsi ya Wasafirishaji Watalii ya ZARA (Zara Tours). Banda la Utalii
la Tanzania ambalo lilisimamiwa na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania, Ottawa
liligawa zaidi ya vipeperushi elfu kumi (10,000) kwa watu
waliolitembelea.
Banda la Tanzani lawavutia wageni mbalimbali ambao hawachelei kufika na kujionea wanayojili.
Balozi
wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Mugendi Zoka (Katikati)
akishirikiana na waonyeshaji kutoa maelezo ya vivutio vya utalii vya
Tanzania. Kulia kwa Mhe. Balozi ni Mke wa Balozi, Bibi Esther Nyanzila
Zoka. Kushoto kwa Mhe. Balozi ni Bw. Salumu Mayombo wa Mamlaka ya
Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Bibi Aziza Bukuku na Desire Masire wa
Ubalozi wa Tanzania, Ottawa.
Afisa wa Ubalozi, Bw. Richard Masalu akiwahamasisha watalii kuitembelea Tanzania.
Watalii
wafurika katika banda la Tanzania. Waonyeshaji wakitoa maelezo ya
vivutio vya utalii vya Tanzania. Kutoka juu ni Bw. Salumu Mayombo wa
Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Bibi Aziza Bukuku na Bw.
Desire Masire wa Ubalozi wa Tanzania, Ottawa; na Bibi Mariam Adam wa
Zara Tours.
Balozi
wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Mugendi Zoka (katikati)
akishirikiana na waonyeshaji kutoa maelezo ya vivutio vya utalii vya
Tanzania. Kushoto kwa Mhe. Balozi ni Bw. Salumu Mayombo wa Mamlaka ya
Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Bibi Aziza Bukuku na Bw. Desire Masire
wa Ubalozi wa Tanzania, Ottwa.
Waonyeshaji
wa banda la Tanzania akipanga mikakati kabla nafuriko ya watu
hayajawavamia. Kutoka kushoto ni Bw. David Mshana na Salumu Mayombo wa
Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro. Anayewafuatia ni
Mwanadiaspora anayeishi Montreal , Bi. Veneranda Mamiro. Katikati ni
Mabalozi wa Tanzania na Kenya, Ottawa, Mhe. Jack Mugendi Zoka na Mhe.
John Lepi Lanyasunya; na kushoto ni Bw. Adam Rashid wa Zara Tours.
Waliotupa mgogo ni watalii.
Mwonyesha
wa banda la Cuba akitoa maelezo kwa Balozi wa Tanzania, Ottawa na
Mwakilishi wa Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka (katikati) alipotembelea
katika banda hilo. Kushoto kwa Balozi ni afisa wa Ubalozi, Bw. Paul J.
Makelele akifuatiwa na mke wa Balozi, Bibi Esther Nyazila Zoka.
Mmoja
kati ya watalii waliowahi kuitembelea Tanzania kwa nyakati mbalimbali
akisifia vivutio vya utalii na utamaduni wa Kitanzania, kwa lugha ya
Kiswahili mbele ya Balozi wa Tanzania, Ottawa, Mhe. Jack Mugendi Zoka.
Balozi
wa Kenya , Ottawa Mhe. John Lepi Lanyasunya (katikati aliyevaa skafu
nyeupe) ni miongoni mwa mabalozi waliotembelea banda la Tanzania. Kulia
kwake ni Balozi wa Tanzania, Ottawa, Mhe. Jack Mugendi Zoka na kushoto
kwake ni Bibi Mariam Adam na Bw. Adam Rashid wa Zara Tours.
No comments:
Post a Comment