Viongozi wa ngazi za juu mkoani Rukwa akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa Chama hicho ngazi ya Mkoa, Zeno Nkoswe wametangaza kujiuzulu nafasi zao kufuatia kutoridhishwa na uteuzi wa wabunge wa viti maalum uliofanywa na viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa.
Viongozi hao wa Baraza
la Chadema wameeleza kuwa mbunge wa viti maalum aliyeteuliwa alikuwa
wakala wa TLP na sio Chadema kama walivyodai.
“Aliyeteuliwa
mpaka sasa ni yule aliyekuwa wakala wa TLP. Kwahiyo huyo anaweza
asiwe mbunge wa viti maalum wa Chadema akawa mbunge wa viti maalum wa
TLP,” alisema Nkoswe na kuongeza kuwa Baraza hilo lilimpendekeza kada wa
Chadema Sumbawanga Mjini lakini haikuwa hivyo.
Katika hatua
nyingine, viongozi hao wamesema kuwa uongozi wa ngazi ya Taifa
walishindwa kutimiza ahadi zao za kuwalipa mawakala waliosimamia
uchaguzi katika maeneo hayo.
Walisema kuwa licha ya kuorodhesha
majina ya mawakala hao ambao wamekuwa wakisubiri fedha kutoka makao
makuu, fedha hizo hazikuwasilishwa kwao hivyo kuwafanya viongozi hao
kugombana na mawakala hao.
No comments:
Post a Comment