Dar es Salaam.
Kasi ya utendaji kazi aliyoanza nayo Rais John Magufuli katika muda wa siku 20 inaonekana kubwa na ya aina yake lakini hivyo ndivyo ilikuwa kwa mtangulizi wake, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, miaka 10 iliyopita.
Kasi ya utendaji kazi aliyoanza nayo Rais John Magufuli katika muda wa siku 20 inaonekana kubwa na ya aina yake lakini hivyo ndivyo ilikuwa kwa mtangulizi wake, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, miaka 10 iliyopita.
Uchunguzi
wa Mwananchi umebaini kwamba katika muda wa siku 20, tangu alipoapishwa
Novemba 5, Rais Magufuli amekonga nyoyo za Watanzania baada ya kufanya
ziara za kushtukiza Wizara ya Fedha na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
akavunja Bodi ya Wakurugenzi ya Muhimbili na kuzuia fedha kutumika kwa
ajili ya sherehe badala yake akaagiza zifanye shughuli za jamii.
Rekodi
zinaonyesha kuwa Kikwete, katika siku zake 20 tangu alipoapishwa
Desemba 21, 2005 alifanya mambo kadhaa makubwa likiwamo la kuunda Baraza
la Mawaziri. Pia, katika kipindi hicho Kikwete aliteua Tume ya Jaji
Musa Kipenka kufanya uchunguzi wa mkasa wa kutekwa na hatimaye kuuawa
kwa wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva
teksi mmoja wa jijini Dar es Salaam katika msitu wa Mabwepande.
Magufuli vs Kikwete
-----> Kuapishwa
Baada
ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumtangaza Dk Magufuli kuwa mshindi
wa uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 kwa asilimia 58.46, Novemba 5
aliapishwa rasmi na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande katika sherehe
zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa kimataifa.
Kwa upande wake
Jakaya Kikwete, baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu
uliofanyika Desemba 14, 2005 kwa asilimia 80 aliapishwa Desemba 21 na
Jaji Mkuu, Barnabas Samatta ili kuanza ngwe ya kwanza ya urais. Mwaka
2010 Kikwete aliapishwa na Jaji Mkuu, Augutino Ramadhani.
------>Uteuzi
Kazi
ya kwanza aliyoifanya Dk Magufuli saa chache baada ya kuapishwa ilikuwa
kumteua George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilhali Kikwete
alimteua Johnson Mwanyika kuwa Mwanasheria Mkuu Desemba 24 yaani siku
tatu baadaye.
------>Ziara wizarani
Hata
kabla hajaunda Baraza la Mawaziri, Magufuli amefanya ziara mbili kubwa.
Novemba 6 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa alitembea kwa miguu
kutoka Ikulu hadi Wizara ya Fedha ambako alipita kwa kushtukiza ofisi
moja baada ya nyingine na baadaye alifanya kikao na watendaji.
Novemba
9 alifanya ziara nyingine ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili ambako alivunja Bodi ya Wakurugenzi, alimwondoa Kaimu
Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk Hussein Kidanto na kuamuru mashine
muhimu za vipimo za CT-Scan na MRI kutengenezwa haraka.
Kikwete
kwa upande wake alisubiri hadi baada ya kuunda Baraza la Mawaziri ndipo
akaanza kutembelea wizara na kuwapa maelekezo maalum. Januari 17
alitembelea Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na kuanika
uozo katika wizara hiyo kisha kuamuru wahusika wa rushwa na urasimu
wafukuzwe kazi na alimwagiza Magufuli aliyekuwa waziri wa wizara hiyo,
kuwafagia walaji wote katika wizara hiyo.
Halafu
alitembelea Wizara ya Elimu ya Ufundi ambako aliagiza mitaala ya zamani
irejeshwe, kisha akatembelea Wizara ya Miundombinu.
------->Kuteua wabunge
Novemba
16, Magufuli alimteua Dk Tulia Ackson na hivyo kuwa mteule wa kwanza
katika nafasi ya ubunge hali iliyotumiwa na chama chake CCM kumpendekeza
agombee nafasi ya Naibu Spika wa Bunge la 11 na akashinda. Kabla ya
uteuzi huo, Dk Tulia alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Katika
siku 20 za kwanza, moja ya kazi kubwa alizofanya Kikwete ilikuwa kusuka
Baraza la Mawaziri. Alitangaza baraza lake lenye mawaziri 60 Januari 4,
2006 na siyo Januari 6 kama ilivyokuwa imetangazwa awali.
------->Waziri Mkuu
Novemba
19, Dk Magufuli amteua Mbunge wa Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa
kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati Kikwete
alifanya uteuzi wa Edward Lowassa kuwa Waziri Mkuu Desemba 29, 2005.
------>Ahutubia Bunge
Novemba
20 Dk Magufuli alifanya mambo mawili mjini Dodoma; kwanza, asubuhi
katika ikulu ndogo ya Chamwino alimuapisha Majaliwa kuwa Waziri Mkuu, na
pili jioni, alilihutubia Bunge. Pamoja na uzuri wa hotuba yake
alisusiwa na wabunge wa upinzani waliokuwa wanapinga Rais Magufuli
kuingia bungeni Dk Ali Mohamed Shein kwa madai si rais halali wa
Zanzibar.
Desemba 30, 2005 Kikwete alifanya kazi mbili;
kwanza, asubuhi alimuapisha Lowassa kuwa Waziri Mkuu, na pili jioni
alilihutubia Bunge. Hotuba yake ilipokewa kwa shangwe kwa vile
alisisitiza kaulimbiu yake ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania, kuwapa
ajira vijana na utayari wake kumaliza mpasuko wa kisiasa Zanzibar.
Hotuba
za viongozi hao kwa kiasi kikubwa zilionyesha utayari wa kuwahudumia
wananchi bila kujali itikadi za vyama, kupiga vita ufisadi, kupambana na
majangili na wauzaji dawa za kulevya na kwamba lengo ni kuhakikisha
Tanzania inasonga mbele kimaendeleo.
------->Tofauti zao
Dk
Magufuli ameonyesha utofauti kivitendo na mtangulizi wake baada ya
kufuta safari za nje, lakini Novemba 20 aliagiza kiasi cha Sh 225
milioni zilizokusanywa kwa ajili ya hafla ya wabunge, zipunguzwe ili
zitumike kununua vitanda kwa ajili ya wagonjwa Muhimbili. Ofisi ya Spika
wa Bunge ilisema kuwa kiasi cha Sh25 milioni tu kilibakizwa kwa ajili
ya hafla hiyo kwa watu wasiozidi 5000.
------>Afuta sherehe
Ukiwa
ni msisitizo wa kupunguza matumizi ya fedha, kwa mara ya kwanza
hakutakuwa na maadhimisho ya Sikukuu ya Uhuru, Desemba 9, badala yake
siku hiyo itatumika kufanya usafi nchi nzima. Tangazo hilo la kufuta
sherehe lilitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue Novemba
23 kwamba ufanyike usafi kukabiliana na tishio la kusambaa ugonjwa wa
kipindupindu
------->Tume ya Uchunguzi
Moja ya hatua alizochukua na kumpa sifa Kikwete katika siku za mwanzo Ikulu ni kundwa kwa Tume Maalum iliyoongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu, Musa Kipenka iliyopewa kazi ya kuchunguza chanzo cha vifo na waliohusika na mauaji ya waliokuwa wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge wilayani Ulanga, Morogoro na dereva teksi mmoja wa Dar es Salaam. Tume hiyo iliundwa Januari 23 na ilipewa siku 21 kukamilisha kazi.
No comments:
Post a Comment