Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla ametembelea uwanja wa ndege
Kilimanjaro(KIA) kujionea ujenzi wa ya upanuzi wa uwanja na shughuli za
uwanja wa ndege Katika kikao cha menejimenti ya kampuni ya uendeshaji
uwanja KADCO mkuu wa mkoa amewapongeza uongozi kwa kuongeza ndege
zinazotua na kuruka, uwezo wakujiendesha kwa kuwa na mapato mazuri na
uwezo wa kudhibiti vitendo haramu vya madawa ya kulevya, usafirishaji
nyara za serikali na ugaidi Pamoja na pongezi hizo mkuu wa mkoa ameagiza
yafuatayo yatekelezwe.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla (pichani juu)akizungumza na menejimenti ya Kadco katika uwanja wa ndege kuhusiana na Uwanja huo usiwe njia ya wapitishaji madawa ya kulevya kwani kuruhusu hilo tunapoteza nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla akitembelea Uwanja
wa Kia na kuwaambia kuwa uwanja huo usiwe njia ya kutorosha nyara za
taifa kwani kufanya hivyo ni kupoteza mapato ya taifa na raslimali za
taifa.
pia Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla ameagiza
menejimenti kuutangaza uwanja huo kimataifa ili uvutie wageni zaidi
kuja kuona vivutio vya utalii tukivyonavyo na kufanya hivyo ni kuongeza
pato la taifa.
Mkuu wa mkoa akiongea na menejimenti ya Kadco leo alipotembelea uwanja wa ndege wa Kia mkoani Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment