WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wakurugenzi wa vitengo na wakuu wa taasisi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) wapate nakala ya hansard ya hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuzindua Bunge la 11, waisome na kufanyia kazi maeneo yote aliyoyaainisha.
“Katibu Mkuu hakikisha umepata hansard ya hotuba ya Mheshimiwa
Rais wakati akizindua Bunge na uhakikishe kila mkurugenzi ana nakala na
kila mmoja wenu lazima ahakikishe anafanyia maeneo ambayo Mheshimiwa
Rais ameyaainisha. Ni lazima tuelewane ni nini tunapaswa tufanye,”
alisema.
Ametoa kauli hiyo jana (JANA) mchana (Jumanne, Novemba 24, 2015) wakati
akizungumza na wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu (TAMISEMI) kwenye mkutano uliofanyika ofisi ndogo ya
TAMISEMI, barabara ya Kivukoni, jijini Dar es Salaam.
“Ninatamani kuona mabadiliko ya utendaji kazi Serikalini katika kipindi
kifupi. Natamani kila mmoja asiridhike na uzembe unaofanywa huku chini.
Ni nyote ni wataalamu, kwa hiyo mnapaswa kudhirisha elimu yenu na ujuzi
mlionao,” aliwasisitizia Wakurugenzi hao.
Alisema kila mkurugenzi na mkuu wa taasisi anapaswa kuongeza usimamizi
na ufuatiliaji wa kazi kwenye sekta yake kwani hilo litasaidia kukidhi
matarajio ya Watanzania ya kuona mabadiliko ya utendaji kazi kwenye
Serikali ya Awamu ya Tano.
“Ninyi wakurugenzi siyo desk officers bali ni field officers. Nataka muweke utaratibu wa kwenda vijijini mkasimamie watu wenu, pia mhimize uadilifu, uaminifu na weledi wa kazi,” alisisitiza.
“Ninyi wakurugenzi siyo desk officers bali ni field officers. Nataka muweke utaratibu wa kwenda vijijini mkasimamie watu wenu, pia mhimize uadilifu, uaminifu na weledi wa kazi,” alisisitiza.
“Mambo ninayotaka mhimize watendaji waliopo chini yenu ni pamoja na haya
yafuatayo: muda wa kuripoti kazini uzingatiwe, muda wa kukaa kazini
uzingatiwe, utokaji kazini kwenda kwenye chai na chakula cha mchana
udhibitiwe, na mipango na malengo ya kazi kwa siku ni lazima yafikiwe,”
alisema.
“Tunataka kujua mtumishi amefanya nini tangu alipoingia ofisini. Suala
siyo kukaa tu ofisini, kwani kuna mtu anakaa ofisini, hajaenda hata
kunywa chai lakini ukiuliza amefanya nini hupati jibu la kueleweka. Sisi
kama vongozi wao ni lazima tujue wanafanya kazi gani wanapokuwa
maofisini,” alisisitiza.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa ameitisha kikao ofisini
kwake kesho (LEO )saa 4 asubuhi akitaka kupatiwa taarifa ni kwa nini mradi wa
mabasi yaendayo kasi (DART) haujaanza kazi hadi sasa.
“Kesho( LEO) saa 4 asubuhi Katibu Mkuu, Mkurugenzi Mkuu DART na watendaji wako mje ofisini. Nataka kupata maelezo ni kwa nini mabasi hayajaanza kazi hadi leo, je ni lini yataanza kazi, je ni nani anakwamisha. Na hata kama ni sheria, ni kwa nini tusiziharmonise ili kuondoa hivyo vikwazo,?” alihoji Waziri Mkuu.
“Kesho( LEO) saa 4 asubuhi Katibu Mkuu, Mkurugenzi Mkuu DART na watendaji wako mje ofisini. Nataka kupata maelezo ni kwa nini mabasi hayajaanza kazi hadi leo, je ni lini yataanza kazi, je ni nani anakwamisha. Na hata kama ni sheria, ni kwa nini tusiziharmonise ili kuondoa hivyo vikwazo,?” alihoji Waziri Mkuu.
“Ninataka kupata haya maelezo kwa sababu Watanzania na hasa wana-Dar es
salaam, wamesubiri kwa muda kuona mradi ukianza kazi ili uondoe kero ya
usafiri. Wao wanajua anayehusika ni TAMISEMI,” aliongeza.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na watumishi na viongozi wa
TAMISEMI, Katibu Mkuu wa OWM-TAMISEMI, Bw. Jumanne Sagini alimweleza
baadhi ya mafanikio na changamoto ambazo wizara hiyo imekabiliana nazo
katika utendaji wake wa kazi.
Kuhusu ujenzi wa vyumba vya maabara kwa ajili ya kuimarisha ufundishaji
wa masomo ya sayansi, Bw. Sagini alisema vyumba hivyo vimeongezeka
kutoka 247 mwaka 2005/2006 na kufikia 6,161 mwaka 2014/2015. Pia alisema
vyumba 4,228 viko kwenye hatua za kukamilika ujenzi wake.
Kuhusu utengaji wa madirisha ya kuhudumia makundi yenye msamaha kama
wazee na watu wenye ulemavu hospitalini na kwenye vituo vya afya, Katibu
Mkuu alisema nayo yameongezeka kutoka madirisha 5,074 mwaka 2010 na
kufikia 7,903 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 55.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, NOVEMBA 24, 2015.
No comments:
Post a Comment