Wanahabarina
mashabiki wa soka wakiwa wamejikusanya ndani ya uwanja huo wa mpira
ambao nje kulitokea mlipuko huo wa mabomu uliouwa watu zaidi ya 120
usiku wa Novemba 13.2015 katika jiji la Paris.
Na Rabi Hume na mashirika ya habari
Polisi
waliokuwa wakikagua mashabiki wa mpira waliokuwa wakiingia uwanjani
katika mchezo wa kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani wameuambia
mtandao wa Wall Street Journal kuwa kuna mshambuliaji wa tukio hilo
alitaka kuingia uwanjani.
Polisi
wamesema kuwa mshambulizi huyo alikuwa na tiketi na alitaka kuingia
dakika 15 baada ya mchezo kuanza lakini walimgundua wakati wakimkagua na
alipofahamu kuwa wamemgundua alikimbia huku akijaribu kulipia mlipuko
wake bila mafanikio.
Polisi
hao wameongeza kuwa mshambulizi alitaka kuingia ndani ya uwanja ili
akafanye shambulizi ndani ya uwanja lakini wakawa wamefanikiwa kulizua
tukio hilo.
Baada
ya kumdhibiti mshambulizi huyo ulisikika mlipuko wa pili nje ya uwanja
huo wa taifa (stade de France) kabla ya mlipuko wa tatu uliosikika
karibu na eneo la McDonald.
Akizungumzia
tukio hilo mshindi wa 2008 wa mchezo kuruka kwa umbali mrefu kwa watu
wenye ulemavu wa miguu, Arnaud Assoumani alikiambia kituo cha Tv cha
L’Equipe kuwa baada ya milipuko hiyo hawakuwa na furaha tena ndani ya
kiwanja na kila mmoja alikuwa na hofu juu ya maisha yake.
“Tulihisi
kuteseka ndani ya uwanja na kila taarifa iliyokuwa ikitujia ilikuwa ya
kutisha zaidi,” alisema Assoumani na kuongeza kuwa “Baadae tukapata
tangazo kuwa wamefungua mlango na tunaweza kutoka niliona watu
wakijaribu kutoka kwa haraka hata kujigonga mlangoni ili waweze kutoka
ila ninaamini hawakuumia”
Nchi
ya Ufaransa inatarajiwa kuandaa mashindano ya Ulaya mwaka 2016 ambapo
michezo 51 itachezwa katika viwanja 10 huku mchezo wa ufunguzi
ukifanyika katika uwanja wa Stade de France hapo Julai 10.2016 na
kuja kutumika tena kwa fainali mwezi mmoja baadae.
Vikosi
vya usalama wakiwa wamemweka chini ya ulinzi mmoja wa watu waliokutwa
eneo ambalo ni hatua chache mmilipuko huo wa mabaomu ulitokea usiku huo
wa Novemba 13.2015.
No comments:
Post a Comment