Kiungo wa timu ya Taifa ya Ufaransa na klabu ya Marseille, Lassana Diarra.
Shambulio
limelotokea usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi katika jiji la Paris,
Ufaransa wakati mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Taifa ya Ufaransa na
Ujerumani umeacha simanzi kwa kiungo wa timu ya Taifa ya Ufaransa na
klabu ya Marseille, Lassana Diarra.
Katika
shambulio hilo ambalo linakadiliwa kuua watu zaidi 150 limepelekea
Diarra kumpoteza binamu yake, Asta Diakote ambae alikuwa moja kati ya
watazamaji waliokuwa katika uwanja wa Stade de France kushuhudia mchezo
huo wa kirafiki.
Diarra
mchezaji wa zamani wa Real Madrid, Arsenal na Chelsea ambae katika
mchezo huo alicheza kwa dakika 80 alisema kuwa binamu yake huyo alikuwa
katika mlango wa G wa uwanja huo.
Baada
ya kumalizika kwa mchezo huo kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika
“Baada ya tukio lililotokea jana Paris na Saint – Deris ni huzuni kwa
hili nisemalo leo”
“Binafsi
nimeathiriwa na shambulizi, binamu yangu Asta Diakite ni mmoja ya watu
wameoathiriwa katika tukio la Jana ambalo limewapata zaidi ya Wafaransa
100 wasio na hata, alikuwa mhamasishaji dada mkubwa”
“Kwa
pamoja tunatakiwa kulindana, tupendane, tuheshimiane na tuwe watu wa
amani. Asanteni kwa msaada na meseji zenu. Tuwe makini na waathirika
wapumzike kwa amani,” alisema Diarra.
Nae
mchezaji mwenzake Diarra wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Antonie Griezman
alitangaza kuwa dada yake alinusurika katika shambulio hilo wakati
akiwa katika ukumbi wa Bataclan wakati akishuhudia bendi ya kutoka
Marekani ya American Rockband Eagles of Death Metal likitumbuiza.
Baada
ya tukio hilo michezo yote nchini Ufaransa imesimamishwa kwa muda na
Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF) limethibitisha kuwepo kwa mchezo wa
kirafiki kati ya timu ya Taifa ya Wingereza na Ufaransa mchezo
utakaochezwa Jumanne katika uwanja wa Wembley London, Wingereza.
No comments:
Post a Comment