Mbunge Mteule wa Jimbo la Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Na Lilian Lundo, MAELEZO-DODOMA
Mbunge
Mteule wa Jimbo la Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema Waziri Mkuu
wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania atatokana na uteuzi
utakaoidhinishwa na Bunge na si taarifa zilizopo sasa katika mitandao
ya kijamii.
Dkt.
Mwakyembe ambaye amewahi kuwa Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya
Awamu ya Nne, alisema kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi, Waziri
Mkuu anateuliwa na Rais ambaye huwasilisha jina hilo kwa Spika wa Bunge
na baadaye kupigiwa kura na Wabunge.
Mbunge
huyo aliyasema hayo leo Jumapili (Novemba 15, 2015) Mjini hapa wakati
alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari kuhusu tetesi zilizopo katika
vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kuhusiana na
jina lake kutajwa kuwa ndiye Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano.
“Mimi
siwezi kuwasemea wananchi na siwezi kusema kuna watu wengi wanasema
hivi, kwani nafasi ya Uwaziri Mkuu haiji kwa njia ya kura ya maoni,
wala kwa njia ya mitandao ya kijamii ni nafasi ya uteuzi
inayoidhinishwa na bunge na ni mamlaka ya Rais wa nchi” alisema Dkt.
Mwakyembe.
Aidha,
Mhe. Mwakyembe aliwataka Watanzania bila kujali itikadi za dini na
vyama vyao wamuombee Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze kuchague
viongozi watakao wajibika na ambao wataendana na kasi ya Mhe. Rais.
Wabunge
wengine waliotajwa kuwepo kwa uwezekano wa kuteuliwa nafasi ya Uwaziri
Mkuu wa Awamu ya Tano ya Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli ni pamoja
na Mhe. William Lukuvi, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo na Mhe. January
Makamba.
No comments:
Post a Comment