WASANII
mbalimbali wa muziki na maigizo pamoja na wadau wengine wa biashara
watajumuika pamoja Triniti, Oyster bay katika tamasha la biashara za
bidhaa mbalimbali, Pop Up Bongo.
Tamasha
hilo linalofanyika kila baada ya miezi mitatu ni la siku moja na mwaka
huu litafanyika tarehe 28 likiwa chini ya udhamini wa kinywaji cha
Smirnoff. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Akizungumzia
kuhusiana na tamasha hilo mmoja kati ya waanzilishi wake, Natasha
Stambuli alisema kuwa milango itafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi na
kuwa linatarajiwa kumalizika saa mbili usiku.
Alisema
kuwa ikiwa ni kuelekea msimu wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya
tamasha hilo linawakutanisha watu mbalimbali na wamiliki wa maduka na
wafanyabiashara za aina mbalimbali.
Alikuwa
inakuwa ni nafasi nzuri kwa watu mbalimbali pia kukutana na mbali na
kufanyika kwa biashara kwenye eneo hilo lakini pia inakuwa ni fursa ya
kuburudika kwa kuwa kutakuwa na muziki na vinwaji hivyo kuongeza furaha
kwa watakaojitokeza.
"Ni
mwishoni mwa mwaka tunaelekea na kama mnavyojua kunakuwa na mambo
mbalimbali wakati tukielekea kufunga mwaka vijana wanataka kujua wapi pa
kununua bidhaa mbalimbali kama nguo na vinginevyo na Pop Up bongo
inawapatia fursa hiyo hapo Novemba 27" alisema Natasha.
Aliongeza
kuwa "kwa mwaka huu wasanii pia wapo ambao watafika kuonana nao wadau
wengine wa bidhaa zinazowahusu kama nguo na nyinginezo na hakuna
kiingilio kabisa.
Alisema
kuwa wafanyabiashara ambao kwa mwaka huu wataonesha bidhaa zao ni
pamoja na Secret Habits, KAYA African Collection, Nuya’s Essence,
HIGHSUPDSM, FT boutique, Branoz Collections, ATSU, Dress Kitenge,
American Nails na wengineo wengi.
No comments:
Post a Comment