Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala akiwa katika ofisi ya Mkurugenzi wa
Manispaa ya Moshi,kuzingumza na watendaji wa Afya na Mazingira.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala akifurahia jambo mara baada ya
kukutana na watendaji wa Halmashauri kuzungumzia juu ya hofu ya Ugonjwa
hatari wa Kipindupindu.kushoto kwake ni kaimu mkurugenzi wa Manispaa
hiyo Jeshi Lupembe.
Baadhi ya watendaji.
Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga akiwa na mmoja wa maofisa wakifuatilia maelelzo yaliyokuwa yakitolewa ofisini hapo.
Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizungumzia changamoto
iliyojitokeza hivi karibuni ya kujaa kwa dampo la kutupa taka hali
iliyosababisha mrundikano wa takataka katika maeneo mbalimbali ya mji wa
Moshi,Hapa alikuwa akitoa agizo taizo hilo kushughulikiwa mara moja.
Baada
ya agizo hilo mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga alifanya ziara
katika dampo lilopo Kaloleni kujinea tatizo lililosabaisha magari ya
kubeba taka kushindwa kuendelea na zoezi hilo.
Katapila likijaribu kusawazisha takataka katika eneo hilo la dampo ili kurahisisha utupwaji wa taka katika eneo hilo.
Wakati
zoezi la kurekebisha barabara katika eneo la dampo likiendelea,mmoja wa
wananchi kkatika eneo hilo alikuwa na shughuli ya kujiokotea vitu
ambayo anadhani vitamsadia katika kujipatia kipato.
Mifugo aina ya Mbuzi pia wamekuwa wakifanya eneo hilo la dampo kama sehemu ya kujipatia chakula.
Wafanyakazi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakizoea taka zilizokuwa
zimerundikana katika eneo la jirani kabisa na soko la Manyema mjni
hapa.
Mkuu
wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga akizungumza namna ambavyo
utekelezaji wa agizo la mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro lilivyoanza ikiwa ni
njia moja wapo ya kukabiliana na Ugonjwa hatari wa Kipindu pindu.
Hivi ndiyo hali iliyokuwa katika soko la MANYEMA.
DC Makunga akijionea hali halisi.
Moja ya dampo likiwa limejaa taka.
No comments:
Post a Comment