Mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali mkoani Tabora zaua watoto wanne. - LEKULE

Breaking

22 Nov 2015

Mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali mkoani Tabora zaua watoto wanne.

Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali mkoani Tabora, jumla ya watoto wanne wamepoteza maisha kwa nyakati tofauti kwa kutumbukia katika madimbwi yaliyojaa maji huku mmoja akiwa na matatizo ya akili, katika wilaya za sikonge na uyui mkoani humo.
Akidhibitisha kutokea matukio hayo, kamanda wa polisi mkoani Tabora kamishina msaidizi Hamis Issa Suleimani amesema kuwa, vifo hivyo ni vya kusikitisha vimesababishwa na familia husika kwani watoto hao kwanza wako chini ya miaka minane, jambo ambalo lingezuirika kama kungekuwepo na uangalifu kwa watoto. 
 
Aidha katika hatua nyingine kamanda Hamisi Suleimani amewataka wananchi wa manispaa ya Tabora ambao wamekuwa wakiibiwa samani zao za ndani ya nyumba, kufika katika kituo cha polisi cha kati kutambua mali zao zilizokamatwa katika msako wa waalifu, ili waziendeleze katika shughuli za kimaendeleo. 
 
Wakati huohuo mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Shabani Kasora mkazi wa Kanyenye, manispaa ya Tabora aliyekuwa akifanya shughuli za kuosha magali, amefariki duni katika kisima alichokuwa amezoea kichota maji kwa ajili ya shughuli zao, katika kile kilichodaiwa kuwa, aliingia kutafuta simu iliyotumbukia humo lakini akiwa amejichanganya kiakili

No comments: