Hospitali
ya rufaa Mbeya ambayo ipo kwenye mchakato wa kubadilisha jina na kuitwa
hospitali ya kanda ya nyanda za juu kusini, inakabiliwa na upungufu
mkubwa wa madaktari bingwa hali ambayo inasababisha utoaji wa huduma
katika baadhi ya maeneo kufanyika kwa kiwango kisichoridhisha.
Kaimu mkurugenzi wa hospitali ya kanda ya nyanda za juu kusini, Dk
Thomas Isdory Matiko amesema kuwa idadi ya madaktari bingwa waliopo kwa
sasa hosptalini hapo ni asilimia 40 tu ya mahitaji ya hospitali hiyo.
Aidha Dk. Matiko ameyataja baadhi ya maeneo yenye upungufu mkubwa
wa madaktari bingwa kuwa kitengo cha mifupa ambacho kwa sasa kina
daktari bingwa mmoja tu licha ya kwamba kutokana na ajali za mara kwa
mara kitengo hicho kwa sasa kina wagonjwa wengi.
Kwa upande wake katibu wa hospitali hiyo, Myriam Msalale amesema
uongozi umechukua hatua kadhaa kukabiliana na tatizo hilo la uhaba wa
madaktari bingwa na kwamba hadi sasa kuna mazungumzo yanayofanyika kwa
ajili ya kupata madaktari kutoka nchini Misri kuja kusaidia kutoa huduma
za matibabu kwa gharama za hospitali hiyo
No comments:
Post a Comment