Mhanga mmoja kati ya 5 wa ajali ya mgodi wa Nyangalata amefariki dunia. - LEKULE

Breaking

22 Nov 2015

Mhanga mmoja kati ya 5 wa ajali ya mgodi wa Nyangalata amefariki dunia.

Mhanga mmoja kati ya watano wa ajali ya mgodi wa dhahabu wa Nyangalata waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama amefariki dunia leo saa sita mchana.
Akithibitisha kifo cha mtu huyo mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kahama Dr.Joseph Ngowi amesema hadi jana usiku afya ya mgonjw huyo ilikua nzuri lakini leo asubuhi alianza kutapika mfululizo na ilipofika saa sita mchana wa leo akafariki dunia.
 
Nao baadhi ya ndugu wa marehemu wamesema wamepokea kifo cha ndugu ya kwa masikitiko lakini wanamshukuru mwenyezi mungu na sasa wanajiandaa kuusafirisha mwili wa ndugu yao kwenda nyumbani kwao Tarime kwa ajili ya mazishi.
 
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama Bw.Vitta Kawawa akidai kuwa halmashuri yake imepokea taarifa za kifo hicho kwa masikitiko kwakuwa walikua wanafanya jitihada kuhakikisha wahanga wote wanapona na kurejea katika familia zao.

No comments: