Chadema Kufungua Kesi Kupinga Agizo la Polisi Kuzuia Kuagwa Mwili wa Alphonce Mawazo. - LEKULE

Breaking

22 Nov 2015

Chadema Kufungua Kesi Kupinga Agizo la Polisi Kuzuia Kuagwa Mwili wa Alphonce Mawazo.



Baada ya zoezi la kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo kushindikana kutokana na jeshi la polisi mkoani Mwanza kupiga marufuku mikusanyiko ya wanachama na wafuasi wa chama hicho kwa madai ya kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu jijini Mwanza, hatimaye viongozi wakuu wa kitaifa wa Chadema pamoja na familia ya marehemu wameamua kwenda mahakamani kesho kutafuta haki yao ya kisheria.
 
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Mwanza  na mwenyekiti wa Chadema taifa Mh. Freeman Mbowe akiwa pamoja na Waziri mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye pamoja na aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) Mh. Edward Lowassa.

Naye Mchungaji Charles Lugiko ambaye ni baba wa marehemu Alphone Mawazo amelaani  kitendo cha askari polisi kwenda hadi nyumbani kwake eneo la Nyegezi na kuwatawanya waombolezaji waliokuwa wamekusanyika nyumbani kwa ajili ya kuuaga  mwili  wa  marehemu Mawazo.

Alphonce Mawazo aliuawa kikatili kwa kukatwa mapanga na mashoka na watu wasiojulikana Novemba 14 mwaka huu katika kijiji cha katoro wilayani Geita.

No comments: