Hofu
huzuni na majonzi vimetanda kwa madereva ambao ni wanachama wa chama
cha madereva nchini waliokuwa wamekusanyika katika chumba cha kuhifadhia
maiti cha hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kupata taarifa kuwa
katibu na msemaji wa chama cha madereva nchini Bwana Rashid Salehe
amefariki dunia baada ya kugua gafla ugonjwa usiojulikana.
ITV ilipofika katika hospilati ya Muhimbili ilikuwa madereva
wameketi mafungumafungu huku wakiwa wamejawana majonzi mazito na kudai
kutoamini kilekilichotokea baada ya kupata taarifa kuwa katibu na
msemaji wao amefariki dunia katika mazingira ya kifo chake ambacho
wamedai kimegubikwa na utata mkubwa na kuomba madaktari kufanya
uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha kifo chake kama anavyobainisha
mwenyekiti wa chama cha maderva nchini Bwana Shaban Mdemu.
Muda mfupi baadae mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck
Sadiki naye aliunga na madereva hao na kuelezea kushitushwa na
kusikitishwa na kifo cha Rashid Salehe na kusema amefariki kipindi
ambacho mchango wake muhimu ulikuwa unahitajika katika kutanzua matatizo
yayowakabili madereva nchini na kulazimika kuagiza jopo la madaktari wa
Muhimbili kufanya uchunguzi wa kina kwa mwili wa katibu huyo wa
madereva ili kujua chanzo na sababu ya kifo chake.
Wiki moja kabla kugua gafla na kufariki kwa katibu na msemaji wa
chama cha madereva nchini Bwana Rashid Salehe ITV ilipata fursa ya
kufanya nae mahojiano juu ya changamoto zinazowakabilia madereva hasa
katika mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC nani hatua gani chama
chake kinachukau.
No comments:
Post a Comment