ALIYEKUWA
mgombea wa Ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
jimbo la Kyela Mbeya,Abraham Mwanyamaki amefungua kesi ya kupinga
matokeo yaliyompa ushindi Dr,Harrison Mwakyembe (CCM) katika mahakama
kuu kanda ya Mbeya akidai yalikuwa na kasoro Lukuki.
Akizungumza
jana na waandishi wa habari kwenye mahakama hiyo,Mwanyamaki alisema Dr,
Mwakyembe hakushinda kihalali katika uchaguzi huo ambapo alipoona
ameshindwa aliliamuru jeshi la polisi kuwatawanya watu kwa kuwapiga
mabomu kisha kujitangazia ushindi kinyume na taratibu.
Alisema
katika mchakato mzima kuanzia kura za maoni Mwakyembe alitoa Rushwa ya
pesa na vitu kadhaa kwa wananchi akiwarubuni kumpa kura wakati wa
uchaguzi ikiwemo kutoa kauli chafu katika kampeni na kuwa wakati wa
majumuisho ya kuhesabu kura alimuamuru mkuu wa polisi kumpiga msimamizi
wake.
Kwa
upande wa mkurugenzi wa uchaguzi ambaye pia ni mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya hiyo,Clement Kasongo,alisema alikuwa na kila
dalili za kuchakachua matokeo hayo baada ya kuingiza vituo hewa ambavyo
havikuwepo kwenye orodha pomoja na mambo mengine.
Mwanasheria
aliyeishika kesi hiyo,Benjamin Mwakagamba kutoka kampuni ya Advocates,
Notaries Public Commissioners for oaths ya jijini Dar es Salaam, alisema
kutokana na kuipitia nakuangalia kasoro hizo ameona kuna umuhimu wa
kufungua kesi akiwa na matumaini ya kushinda kutokana na mazingira
yenyewe.
Alisema
mteja wake amefungua kesi ya kihistoria namba 2 ya mwaka 2015
akiwashitaki watu watatu ambao ni mkurugenzi wa tume ya Uchaguzi
Clement Kasongo, namba 2 ni Harrison Mwakyembe na watatu ni mwanasheria
wa halmashauri kwa kukiuka taratibu za uchaguzi wakishirikiana
kuchakachua matokeo.
Alisema
endapo haki itatendeka anauhakika wa kushinda kesi hiyo na endapo haki
haitatendeka watakata rufaa kwenye mahakama za juu kwa kuwa ushahidi
wanao jinsi Dr,Mwakyembe alivyopora ushindi huo akidaiwa kutumia cheo
chake cha uwaziri kulitumikisha jeshi la polisi kuvunja kanuni za
uchaguzi.
Wananchi
kwa upande wao wakiongozwa na Merry Mwakipesile walisema wamesafiri
kutoka wilayani kyela hadi mkoani Mbeya kuhakikisha kesi hiyo
inafunguliwa ambapo alisema wao kama wananchi wanao ushahidi wa kutosha
jinsi Mwakyembe na Tume walivyojipa ushindi huku wananchi wakipigwa na
kuteswa.
Alisema
kutokana na mazingira ya jimbo la Kyela wananchi walivyokuwa wakimzomea
kila kona Dr,Mwakyembe baada ya kuwa mmoja kati ya wabunge mizigo
nchini alivyolitelekeza jimbo hilo likiwa hoi,alijipanga kwa gharama
kubwa ya kifedha kuhakikisha anashinda kwa nguvu.
Alisema
licha ya kutumia kila njia ya kuhakikisha anashinda,lakini wao
walimchagua mgombea wa chadema Abraham Mwanyamaki kwa kumpa kura za
mtikisiko na kuwa cha ajabu wakashangaa wanapigwa mabomu bila sababu
huku Mwakyembe akijitangaza mwenyewe kuwa ameshinda.
Debora
Mwakipesile mkazi wa Kyela,alisema yeye ni mmoja wa wahanga walioteswa
na kudharirishwa na jeshi la polisi na kuvunjwa mkono baada ya kukamatwa
na kutiwa nguvuni huku baadhi ya askali wakimdharirisha kwa shinikizo
la Mwakyembe.
Alisema
kutokana na hali hiyo wao kama wananchi hawapo tayari kufanya kazi na
Mwakyembe kwa kuwa sio chaguo lao ni chaguo la serikali na kuwa mbunge
wao wanayemhitaji ni Abraham Mwanyamaki.
No comments:
Post a Comment