TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
UBOMOAJI
WA NYUMBA MANISPAA YA KINONDONI
Manispaa ya Kinondoni
kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi
na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa
nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.
Maeneo yaliyotengwa mijini kwa matumizi ya
umma ikiwa ni pamoja na maeneo ya wazi, njia za miundombinu na huduma nyinginezo
za umma, mara kwa mara hutumiwa vibaya au kuvamiwa na waendelezaji binafsi
hivyo kuukosesha umma manufaa yaliyokusudiwa.
Tamko Na. 6.6.1 la Sera
ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
i.
Serikali itahakikisha kwamba maeneo yote
mijini yaliyotengwa kwa shughuli za umma yanatumika kwa shughuli zilizokusudiwa
na yanalindwa ili yasivamiwe.
Tamko Na. 8.2.1 la Sera
ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
ii.
Serikali za mitaa zitawajibika
kushirikiana na Wizara ya Ardhi kuhakikisha usimamizi mzuri wa ardhi katika
maeneo yao.
Sera ya Taifa ya Ardhi
imebainisha sababu inayopelekea Wizara kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni
kuendesha zoezi hili la ubomoaji.
Ubomoaji huu utahusisha
nyumba zote zilizojengwa
a)
Bila kibali cha ujenzi
b)
Bila kufuata michoro ya mipango miji
c)
Bila kufuata matumizi ya ardhi (maeneo
ya wazi)
Zoezi hili la ubomoaji
litaendeshwa na Manispaa ya kinondoni na Wizara ya Ardhi itasimamia sera za
ardhi na taratibu za uendelezaji kuhakikisha zinafuatwa na kila mmiliki wa
ardhi.
Maeneo ambayo ujenzi
wake umekiuka matumizi kusudiwa na yatahusika na ubomoaji huu ni Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni –
Biafra. Kazi hii inatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia jumatano tarehe
18/11/2015 hadi ijumaa tarehe 20/11/2015.
No comments:
Post a Comment