Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo |
ASKARI
78 wa usalama barabarani Mkoa wa Mwanza, wameondolewa katika nafasi zao
na kupangiwa kazi nyingine katika vitengo mbalimbali kutokana na utovu
wa nidhamu. .
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo,
akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema mabadiliko hayo
yamefanywa baada ya askari hao kujulikana hawafuati maadili na sheria za
jeshi hilo.
Mkumbo
alisema kuwa askari waliondolewa nafasi hizo na kupangiwa vitendo
vingine ni 78, huku akisema kwamba wilaya ambayo haijafanyiwa mabadiliko
ni Ukerewe kati ya saba za mkoa huo.
“Tumefanya
mabadiliko haya ni ya kawaida tu, tumefanya hivyo ili kuleta utendaji
wenye tija, baada ya kubaini kuna mapungufu kwa askari hao na
tusingeendelea kuwa nao kwa kuwa ni watovu wa nidhamu.
“Wilaya
ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni Nyamagana askari 19, Ilemela 23,
Sengerema 15, Magu 15, Misungwi na Kwimba mmoja (1), wilaya ambayo
haijaguswa ni Ukerewe,” alisema Mkumbo.
Hata
hivyo Mkumbo alisema kuwa kabla ya kufanyika kwa mabadiliko hayo,
walianza kutoa mafunzo kwa askari waliochukua nafasi hizo, kabla
hawajaingia barabarani.
Mkumbo
alisema kuwa kabla ya mabadiliko hayo mkoa wa Mwanza ulikuwa na trafiki
249, na kwamba walioondolewa katika nafasi hizo ni askari wa kawaida na
vyeo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment