Mgeni
Rasmi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Prof. Adolf Mkenda
akihutubia wadau mbalimbali wa takwimu katika maaadhimisho ya Siku ya
Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa
na kauli mbiu ya "Takwimu Bora kwa Maisha Bora".
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya
utangulizi katika katika maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika
yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu
ya "Takwimu Bora kwa Maisha Bora".
Mkuu
wa Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano Dkt. Carina Wangwe
kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA) akielezea umuhimu wa kujiunga katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii
wakati wa maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo
Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya "Takwimu Bora
kwa Maisha Bora".
Mkuu
wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof. Innocent Ngalinda
akielezea umuhimu wa takwimu rasmi katika kupanga na kutathmini programu
mbalimbali za maendeleo nchini wakati wa maaadhimisho ya Siku ya
Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa
na kauli mbiu ya "Takwimu Bora kwa Maisha Bora".
Baadhi
ya wadau mbalimbali wa takwimu wakifuatilia kwa makini matukio
yaliyokuwa yakiendelea kwenye maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika
yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu
ya "Takwimu Bora kwa Maisha Bora".
Mwenyekiti
wa Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Prof. Milline Mbonile akiwa katika
picha ya pamoja na viongozi wa ofisi hiyo pamoja na viongozi wa Chuo
cha Takwimu Mashariki mwa Afrika baada ya kumaliza maaadhimisho ya Siku
ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo
yameongozwa na kauli mbiu ya "Takwimu Bora kwa Maisha Bora". (PICHA ZOTE
NA VERONICA KAZIMOTO).
Wizara,
Idara, Wakala, Taasisi za Serikali, Mashirika yasiyokuwa ya Serikali na
Wadau wa Maendeleo wametakiwa kutumia takwimu zinazotolewa na Ofisi ya
Taifa ya Takwimu katika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya
maendeleo hapa nchini.
Akizungumza
katika Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa
matumizi ya takwimu bora ndio msingi katika utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo.
“Leo
tunasherehekea Siku ya Takwimu Afrika, siku ambayo inatukumbusha umuhimu
wa Takwimu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya taifa letu.
Ukiwa na takwimu bora utaweza kutoa huduma zilizo bora,” amesema Prof.
Mkenda.
Prof.
Mkenda amesema uwepo wa takwimu bora zinazoonesha mahitaji halisi ya
wananchi ndio dira katika utaoji wa huduma muhimu za kila siku pamoja na
upangaji na utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo ya kitaifa.
“Maadhimisho
haya leo yanazitaka Serikali zetu kuimarisha mifumo ya kitakwimu kwa
kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ya ukusanyaji, uchambuzi na
usambazaji wa Takwimu. Serikali kwa upande wake itahakikisha inaiwezesha
Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuwekeza katika teknolojia ya kisasa zaidi
ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo ya ukusanyaji wa Takwimu
bora na kwa wakati,” amesisitiza Prof. Mkenda.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina
Chuwa amesema Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka huu imelenga katika
kuufahamisha umma kuhusu umuhimu wa Takwimu bora kwa maendeleo yao na
Taifa kwa ujumla.
“Siku
hii ya Takwimu Afrika ni muhimu sana kwetu sisi hasa watakwimu kwani
tunaitumia kuelimisha umma juu ya umuhimu wa Takwimu katika mustakabali
wa maendeleo ya Taifa,” amesema Dkt. Chuwa.
Dkt.
Chuwa amesema kupitia maadhimisho haya yanayoongozwa na kauli mbiu ya
"Takwimu Bora kwa Maisha Bora", itawasaidia wananchi kutambua kuwa uwepo
wa takwimu bora ndio njia ya upatikanaji wa maendeleo stahiki.
Nae
Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),
Dkt. Carina Wangwe amesema wakiwa kama watumiaji wakubwa wa Takwimu
zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika utekelezaji wa majukumu
yao ndio wanathamini mchango wa takwimu rasmi katika kupanga mipango ya
maendeleo.
“Sisi
ni wadau wakubwa na watumiaji wa takwimu zinazotolewa na Ofisi ya Taifa
ya Takwimu, leo hii tupo hapa ili kushirikiana na ofisi hii ili
kuhakikisha teknolojia ya kisasa inatumika katika uboreshaji wa Takwimu
na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii,’ amesema
Dkt. Wangwe.
Siku
ya Takwimu Afrika huadhimishwa tarehe 18 Novemba, kila mwaka, Kwa hapa
Tanzania maadhimisho haya yamefanyika Novemba 23, 2015 ambapo kauli mbiu
ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “Takwimu Bora kwa Maisha Bora".
No comments:
Post a Comment