Ofisa
michezo wa wilaya ya Manyoni, Salumu Mohamedi Mkuya akiongoza ratiba ya
michezo ya tamasha iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari
Kilimatinde,wilayani Manyoni.
Mwenyekiti
wa CWT Wilaya ya Manyoni, Jesca Mununo na Katibu wa CWT Wilaya ya
Manyoni, Nalea Nyamuyo wakibadilishana mawazo wakati wa tamasha la
michezo kwa shule za msingi na sekondari za tarafa ya
Kilimatinde,wilayani Manyoni.
Mwenyekiti
wa CWT Mkoa wa Singida, Arani Jumbe ( wa nne kutoka kulia), Mwenyekiti
wa CWT Wilaya ya Manyoni, Jesca Mununo (wa tano kutoka kulia),Ofisa
michezo wa wilaya ya Manyoni, Salumu Mohamedi Mkuya (wa tano kutoka
kulia), Katibu wa CWT Wilaya ya Manyoni, Nelea Nyamuyo (wa tatu kutoka
kushoto) na Katibu wa CWT Mkoa wa Singida, Kitundu (wa pili kutoka
kulia).
Timu ya soka ya shule ya Mtakatifu Johns ya Kilimatinde wakijiandaa kucheza mchezo wao na timu ya soka ya Kilimatinde.
Baadhi
ya walimu wa shule ya msingi zilizokuwa zikishiriki katika tamasha la
michezo wakishangaa jinsi goli lilivyoingia kwenye moja ya timu
zilizokuwa zikishiriki kwenye tamasha hilo.
Mwalimu
Mwahija wa shule ya msingi Kilimatinde (mwenye mtandio mweupe)
akipongezana na mwalimu mwenzake baada ya timu ya shule yao kupata goli
la kuongoza.
Na, Jumbe Ismailly, Manyoni
HALMASHAURI
za wilaya, Miji, Manispaa na Majiji nchini zimeshauriwa kuhakikisha
zinatenga maeneo ya wazi kwa ajili ya viwanja vya michezo, ili viweze
kuwasaidia watoto kufanya mazoezi na kuibua vipaji vyao mbalimbali vya
michezo.
Ushauri
huo umetolewa na Katibu wa CWT Wilaya ya Manyoni,Nelea Nyang’uyo kwenye
tamasha la michezo lililoandaliwa na Chama Cha Walimu Tanzania Mkoa wa
Singida kwa kushirikiana na Mradi wa Elimu Kupitia Michezo(ETS) kwa
ajili ya kuibua vipaji vya michezo pamoja na kuwaandaa wachezaji wa siku
za baadaye,lililofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari
Kilimatinde,wilayani Manyoni.
Huku
akitoa mifano katibu huyo alifafanua kwamba baadhi ya shule zilizopo
mjini Manyoni zimekuwa na maeneo finyu kutokana na kutotengewa maeneo
kwa ajili ya michezo,jambo ambalo huwafanya watoto kukosa eneo la
kufanyia mazoezi na hivyo kutokuwepo maandalizi ya wachezaji wa siku za
baadaye.
“Pamoja
na maandalizi mazuri ambayo yamefanyika lakini ni vizuri nitoe wito
wakati huu kwamba michezo ilishakuwa ni burudani na inaandaa akili kwa
ajili ya mwanafunzi kupokea elimu”alisema katibu huyo wa CWT wilaya ya
Manyoni.
Kwa
mujibu wa Nyang’uyo ni vizuri kwa Halmashauri zote nchini,hususani
Halmashauri yao ya Manyoni wakahakikisha wanatenga maeneo wazi kwa ajili
ya viwanja vya michezo kwa sababu maeneo yaliyo mengi yapo finyu na
hata shule zingine hazijatengewa maeneo ya kutosha,hasa shsule zilizopo
katikati ya mji,katika Halmashauri ya wilaya ya Manyoni hazina viwanja
vya michezo.
Aidha
katibu huyo alibainisha kwamba kutokana na shule hizo kutokuwa na
maeneo na viwanja vya michezo jambo linalopelekea watoto kukosa eneo la
kufanyia mazoezi.
“Hata
wachezaji wakubwa wa kimataifa tunaowasikia leo na kuwaona wametokana
na maandalizi mazuri kuanzia ngazi ya chini,kwa hiyo nitoe wito ya
kwamba Halmashauri zote nchini,hususani Halmashauri ya wilaya ya Manyoni
maeneo ya wazi yatengwe kwa ajili ya viwanja vya michezo ili watoto
waweze kupata fursa nzuri ya kushiriki michezo”alisisitiza Nyang’uyo.
Kwa
upande wake Ofisa michezo wa wilaya ya Manyoni,Salumu Mohamedi Mkuya
alitumia fursa hiyo pia kutoa wito kwa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni
kuangalia uwezekano wa kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya michezo
ili Halmashauri hiyo iweze kuendelea kufanya vizuri zaidi katika michezo
mbali mbali wanayoshiriki.
“Wilaya
yetu ya Manyoni imekuwa ikishika nafasi ya ubingwa wa mkoa kwenye
michezo ya Umitashimta mara tatumara tatu kwenye ubingwa wa umitashimta
kimkoa na kweneye mradi huu ya Elimu Kupitia Michezo (ETS) unaofadhiliwa
na nchi ya Finland pamoja na CWT nao tumeshika ushindi wa kwanza mara
tatu kimkoa mfululizo”alibainisha Mkuya,
Hata
hivyo pamoja na kusisitiza utengwaji wa maeneo ya wazi kwa ajili ya
viwanja vya michezo,lakini Mkuya hakusita pia kuwakumbusha wazazi na
walezi wa wanafunzi hao kuwahamasiaha vijana wao kwa kupenda michezo,na
wao wenyewe wawe mstari wa mbele kuhudhuria kwenye matamasha ya michezo
ya vijana wao inapofanyika.
“Jingine
naomba nitoe wito kwa Halmashauri zetu za wilaya pamoja na kutenga
bajeti za michezo lakini zijitahidi kuongeza bajeti kwa ajili ya michezo
ili wilaya yetu iweze kushiriki katika maeneo yote ya michezo,ikiwemo
Umistashimta”alisema.
Naye
Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Singida,Arani
Jumbe alifafanua kuwa mradi huo ulioanza mwaka 2007,mpaka mwaka 2011
ulikuwa ukitoa msaada wa vifaa vya michezo kwa shule za msingi na
kuanzia 2012 hadi 2014 ulikuwa kwenye shule za sekondari na hivi sasa
wanatarajia kuanza kutoa vifaa hivyo kwa shule za watu binafsi.
No comments:
Post a Comment