Kikosi cha brasband cha Magereza kikiongoza Maandamao kuelekea uwanjani kwenye mahafali hayo ya Kumi na Tatu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na ya Tatu kwa kampasi ya Mbeya . |
Baadhi ya wahadhiri wa Taasisi hiyo ya Uhasibu (TIA) Kampasi ya Mbeya wakiandamana kuelekea uwanjani tayari kwa mahafali hayo . |
Wahitimu wakiwa katika maandamano hayo ya Mahafali ya kumi na Tatu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na ya Tatu kwa Kampasi ya Mbeya. |
Baadhi ya wahitimu wa Uhasibu (TIA) kampasi ya Mbeya |
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt .Joseph Kihanda akizungumza kwenye mahafali ya Kumi na tatu ya Taasisi na ya Tatu kufanyika katika Kampasi ya Mbeya. |
Mgeni rasmi Ndugu Nyirembe Munasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ambaye pia alimwakilisha Waziri wa Fedha katika mahafali hayo ya Taasisi ya Uhasibu (TIA) Kampasi ya Mbeya. |
Wahitimu wa Masomo ya Uhasibu Katika Taasisi hiyo wakisikiliza kwa umakini nasaha kutoka kwa mgeni rasmi . |
Kikundi cha ngoma za asili kutoka Ilemi jijini Mbeya kikitoa burudani katika mahafali hayo . |
Mgeni rasmi Nyirembe Munasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya akitoa zawadi kwa washindi walio fanya vyema katika masomo yao. |
Baraza
la Taifa la Elimu ya ufundi (NACTE)limetoa kibali kwa taasisi ya
Uhasibu Tanzania (TIA) kampasi ya Mbeya ili kuongeza kozi nyingine za
shahada ya Masoko na uhusiano kwa umma (Bachelor Degree in Marketing and
public Relation kwa mwaka wa masomo wa 2015-16.
Aidha
baraza hilo pia limetoa kibali kwa kuanzishwa kwa kozi nyingine ya
shahada ya uhasibu wa fedha za umma (Bachelor Degree in Public Sector
Accounting and Finance) kwa mwaka huu wa masomo.
Kauli
hiyo imetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania
Dkt.Joseph Kihanda kwenye mahafali ya kumi na Tatu ya Taasisi na y a
tatu kufanyika katika kampasi ya Mbeya.
Amesema
katika mwaka wa masomo wa 2014-2015 kufuatia maombi ya muda mrefu ya
wadau wake kampasi ya mbeya ilianza kutoa kozi za shahada ya uhasibu na
shahada ya Ununuzi na Ugavi ambazo mwitikio wake umekuwa mkubwa hivyo
kulazimika kuomba kibali cha kuanzisha kozi nyingine ambazo tayari
baraza hilo limekwisha toa kibali
.Amesema
kuanzishwa kwa kozi hizo kumeiwezesha kampasi ya Mbeya kuwabakiza
wanafunzi wanaohitimu kozi za Stashahada katika fani husika ambao hapo
awali walilazimika kuhamia vyuo vingine vinavyotoa kozi hizo kwenye
ngazi ya shahada na hivyo kuikosesha Taasisi mapato.
Aidha
Dkt Kihanda amesema kuwa kuanza kwa kozi hizo pia kutawawezesha wakazi
wa mbeya na mikoa mingine ya jirani kupata fursa ya kujiendeleza
kitaaluma Katika ngazi ya shahada kwani masomo yanatolewa katika mfumo
wa kutwa na jioni hivyo kukidhi kiu ya wengi.
Hata
hivyo amesema kampasi ya Mbeya imejiimarisha sana katika utoaji wa
elimu yenye ubora ili kuwawezesha wahitimu kufanya vizuri katika masomo
yao ya baadae na katika sehemu zao za kazi.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya wizara ya fedha Profesa
Isaya Jairo amesema bodi hiyo itashirikiana na uongozi wa TAASISI
kuishauri Wizara ya Fedha kuitengea fedha za kutosha kwa ajili ya
kuboresha miundo mbinu mbalimbali pamoja na vitendea kazi.
Katika
mahafali hayo, jumla ya wanafunzi 1689 wa stashahada na stashahada za
udhamili katika fani mbalimbali wanahitimu masomo yao ambapo kati yao
wasichana 851 na wanaume 838
No comments:
Post a Comment