Mratibu wa Magonjwa ya Mlipuko Mkoa wa
Dar es Salaam, Vicktoria Bulla (kulia), akizungumza na waandishi wa
habari na wadau wa afya wakati akifungua semina ya siku moja ya ugonjwa
wa kipindupindu Dar es Salaam jana, kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam ambaye alikuwa mgeni rasmi. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Elimu ya Afya kwa Umma, Hellen Semu na Mkurugenzi Msaidizi
Kitengo cha Ufuatiliaji wa Magonjwa ya Mlipuko wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii, Dk.Janeth Mghamba. Semina hiyo iliandaliwa na wizara
hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO)
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.
Ofisa Habari wa Wizara ya Afyaaaa na
Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura (kulia), akibadilishana mawazo na
mwenzake katika semina hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.
Mada mbalimbali kuhusu ugonjwa huo na magonjwa ya mlipuko zikiendelea kutolewa.
Semina ikiendelea.
Wadau wa Afya wakiwa kwenye semina hiyo.
WANANCHI wa jiji la Dar es Salaam
asilimia 70 kati yao wanatumia maji yasiyo salama ambayo yanachangia kwa
kiwango kikubwa kukithiri kwa magonjwa ya mlipuko.
Hayo yalibainishwa Dar es Salaam juzi na
mtaalam wa afya kutoka idara ya kinga kitengo cha afya na mazingira wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Theophil Likingaga katika
semina ya waandishi wa habari ya siku moja iliyoandaliwa na wizara hiyo
kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyohusu ugonjwa wa
kipindupindu.
Dk. Likingaga alisema asilimia hiyo
kubwa ya watanzania kutumia maji yasiyo salama imetokana na Shirika la
Maji safi na Taka (DAWASCO), kuhudumia asilimia 30 tu ya wananchi wa Dar
es Salaam hivyo kuwa changamoto.
Alisema pia asilimia 15 tu ya wananchu
wa Dar es Salaam ndiyo waliounganishwa kwenye mfumo wa maji taka hivyo
kyfanta tatizo la uhaba wa maji safi na utunzaji wa mazingira kuwa
kubwa.
"Hayo ndiyo baadhi ya maeneo ambayo
tumeyaona pia suala la uuzaji matunda kiholela, biashara za vyakula pia
imekuwa ikichangia kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu," alisema
Dk.Likangaga.
Alisema wizara hiyo imejitahidi
kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu kwa kugawa dawa za kusafisha maji
pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.
Likangaga alisema serikali kupitia
DAWASCO imejitahidi kufunga vioski katika maeneo mbalimbali na kusambaza
maji kwa kutumia magari ili wananchi wapate maji safi na salama.
Kwa upande Mtaalam wa Maabara ya Taifa,
Dk.Theophil Malibiche alisema tangu ugonjwa wa kipindupindu uanze Agosti
15 mwaka huu, wamefanya vipimo 1071 ili kubaini vimelea vya
kipindipindu.
Alisema kati ya hizo sampuli 668 sawa na asilimia 62 zimebainika kuwa na vimelea vya kipindupindu.
Kwa upande wake, Ofisa Afya wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Emmanuel Mwandepa alisema serikali inaendelea kuangalia
mbinu mbadala ya kutoa huduma ya maji safi kwa wananchi.
Alisema kutokana na mkakati huo
wameanzisha kampeni yq nyumba kwa nyumba ambayo itakuwa inakagua
mazingira pamoja na ubora wa visima vya maji.
Aliongeza kutokana na mpango huo visima vifupi vya maji vitafungiwa ili kupunguza ugonjwa wa mlipuko.
No comments:
Post a Comment