Serikali wilayani Geita na Polisi Mkoa wa Mwanza, wamepiga marufuku wanachama na wafuasi wa Chadema kukusanyika kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo (pichani).
Akizungumza
ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo
alisema wamezuia mikusanyiko ya aina yoyote kutokana na kuwapo kwa
mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Shughuli
hizo za kuaga mwili zimepangwa kufanyika kati ya leo na kesho kwenye
Viwanja vya Furahisha, au ofisi za Chadema Kanda ya Ziwa.
“...
hatukubali mikusanyiko yoyote kutokana na kuwapo mlipuko wa ugonjwa wa
kipindupindu. Kama ulinzi wa kusindikiza mwili kutoka Bugando hadi Geita
tutawapatia ili wakafanyie taratibu za mazishi huko siyo hapa, ” alisema.
Mkumbo alisema kutokana na mikusanyiko hiyo, yapo makundi yamejipanga kutumia mwanya huo kufanya uhalifu.
Hata
hivyo, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Nyamagana, Japhet Nungwana
alisema tayari walikuwa wameomba Uwanja wa Nyamagana kufanya ibada ya
kumuaga Mawazo.
Alisema
hawajapokea taarifa yoyote ya kuzuia mikusanyiko hiyo na kwamba, kama
wataona siyo vizuri kutumia uwanja wao watafanyia ibada katika ofisi zao
za Kanda.
“Hatuendi
kufanya vurugu au mkutano, tunafanya ibada ya kumuaga ndugu yetu ila
wakituzuia uwanja wao tutatumia ofisi zetu za Kanda,” alisema Nungwa na kuongeza:
“Hatuwezi
kuacha kumuaga kwani yule alishawahi kuwa kiongozi mkoani hapa, hivyo
kushindwa kufanya ibada ya kumuaga tutakuwa hatujatenda haki. Iwapo
wanazuia kwa sababu ya kipindupindu kwa nini hawajazuia ibada na
mikusanyiko ya watu misikitini au makanisani?”
Kaimu
Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza, Onesmo Rwakyendela alisema kwa takriban
miezi miwili, wamepata wagonjwa 422 wa kipindupindu na 18 wamepoteza
maisha.
“Kwa
sasa Wilaya ya Ilemela ina wagonjwa watano, Sengerema na Ukerewe mmoja
mmoja, niwatake wananchi kutofanya mikusanyiko isiyo ya lazima maana
huwezi kujua nani ana vimelea vya ugonjwa huo,” alisema Dk Rwakyendela.
Geita pia Marufuku
Mkuu
wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie amepiga marufuku shughuli ya kuaga
mwili huo iliyokuwa imepangwa kufanyika kesho akisema Mawazo si
kiongozi wa kitaifa wala mkazi wa mjini hapa.
Akizungumza ofisini kwake jana, Mangochie alisema: “Hapa
hana nyumba wala siyo kiongozi wa kitaifa, hivyo msiba wake unatakiwa
upelekwe nyumbani siyo kuagwa kwenye eneo la hadhara, hapa siyo kwake.”
Alisema
ameona kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook mtu mmoja akitoa taarifa
za mazishi kuanzia Mwanza halafu Geita na kwamba, hiyo siyo sahihi na
amepiga marufuku shamrashamra zote kwenye msiba huo.
Hata
hivyo, Katibu Msaidizi wa Chadema wa Jimbo la Geita, George Anthony
alisema chama hicho hakijapata taarifa za zuio hilo na kwamba wametimiza
taratibu zote za kuomba kibali polisi na Serikali walipewa.
“Tumekabidhi
barua na kuongea nao ana kwa ana wameturuhusu na kutupa Uwanja wa
Magereza, sasa sisi ratiba yetu ya kumuaga Jumapili ipo palepale huyu ni
kiongozi wa mkoa na kitaifa wananchi wana haki ya kumuaga,” alisema Anthony.
Alisema ratiba yao inaonyesha kuwa ataagwa mjini Geita na baadaye Katoro, kisha kijijini kwake Chikombe.
DC alaani mauaji
Awali, Mangochie alisema Serikali ilipokea kwa masikitiko msiba huo na kulaani mauaji hayo ya kinyama na kikatili.
“Nitoe
pole kwa familia ya Mawazo pia kwa chama, kwa kuondokewa na kiongozi
wake mimi na viongozi wenzangu tumepokea kwa masikitiko makubwa, nalaani
kitendo kisichokubalika cha kumshambulia na kusababishia kifo,” alisema.
Alisema
zipo taarifa za upotoshaji wa kifo hicho zinazotolewa ambazo siyo za
kweli, hivyo kuwataka wananchi kuachana nazo na kusubiri taarifa za
uhakika kutoka polisi
No comments:
Post a Comment