UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umesema mipango yao ya kutomruhusu Rais Dk. John Magufuli kulihutubia Bunge akiwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, imefanikiwa.
Mwenyekiti wa Umoja huo, Freeman Mbowe, alisema
jana kuwa walimua kuzuia Rais Magufuli asihutubie Bunge kwa vile Dk.
Shein, muda wake wa kuwa rais ulikwisha tangu Novemba 2 mwaka huu kwa
hiyo hakustahili kuhudhuria Bunge hilo.
Alisema kuwa waliamua
kufanya vile wakiamini kuwa ilikuwa sehemu muafaka ya kufikisha kilio
chao kutokana na wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano ule, wakitokea
katika nchi za jumuiya ya kimataifa.
“Tulishangaa
kumuona Dk. Shein, Pandu Amiri Kificho na Makamu wa Pili wa Rais wakiwa
ndani ya Bunge wakati kikatiba hawana uhalali,” alisema Mbowe.
Alisema,
baada ya kitendo kile hivi sasa umoja wa vyama hivyo, unatarajia
kukutana ili kupeana mikakati ya kuendeleza mapambano ya ndani na nje ya
nchi ya kudai haki.
“Uchaguzi wa Zanzibar hauwezi kutenganishwa kikatiba au kisiasa na uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya muungano,” alisema Mbowe.
Mbowe alisema Ukawa hawako tayari kuinajisi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuruhusu viongozi wasio halali kuingia bungeni.
Aidha, Mbowe alisema
walitaka shughuli ya ufunguzi rasmi wa Bunge isitishwe kwa sasa na
kuahirishwa hadi hapo Rais halali aliyechaguliwa na wananchi wa
Zanzibar, Seif Sharrif Hamad, atakapotangazwa rasmi na kuapishwa.
Naye Mwenyekiti Mwenza, James Mbatia, alisema
haijawahi kutokea katika historia ya Bunge tangu nchi hiyo ilipopata
uhuru kwa vyombo vya dola kuingia ndani ya bunge na kuwatoa wabunge kwa
nguvu.
“Wakati
sisi tunatafuta majadiliano mezani ilikumaliza mgogoro huu wenzetu
Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameamua kutumia majeshi kukandamiza
demokrasia,” alisema Mbatia.
Mbatia alisema kuwa hawatakaa kimya bali wataendelea kupigania matakwa ya wananchi hususan kwa upande wa Zanzibara.
“Kuna
mambo mengi yanafanywa hovyo na CCM na wapinzani wamekuwa wakivumilia
kwa sababu ya kumpenda mama Tanzania lakini hivi sasa wasijaribu
kuharibu amani, utulivu na mshikamano uliopo,” alisema.
Mbatia, alisema
kwa kawaida mtu anapodhulumiwa haki yake kila mara matokeo yake
anachoka kwa hiyo kuna siku ataifuta haki yake hata kwa kusababisha
kumwaga damu.
Naye Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema
Umoja wa Katiba ya Wanachi (Ukawa ) wamesikitishwa na kitendo cha
serikali ya CCM kuonesha wazi jinsi walivyobaka na kuikanyaga demokrasia
nchini.
Alitoa kauli hiyo aipokuwa akizungumza na mwandishi wetu muda
mfupi baada ya kutoka bungeni baada ya kufukuzwa na Spika wa Bunge, Job
Ndugai baada ya wabunge wa umoja huo kupinga kitendo cha kuruhusiwa kwa
Rais wa Zanzibar kuwa sehemu ya Bunge.
Lissu alisema
imeonesha wazi kuwa serikali ya CCM ilivyo kuwa ikitumia mabavu ya
kuvunja sheria waziwazi sambamba na kuvunja kanuni za bunge jambo ambalo
ni hatari kwa afya ya nchi.
Akizungumzia kutoka kwao nje ya ukumbi wa Bunge alisema
serikali ya CCM kwa kutumia kiti cha Spika walionekana kupanga mbinu
chafu za kuwazima wabunge wa Ukawa ili wasiweze kufikisha hoja zao mbele
za wananchi kupitia bunge hilo.
“Unaweza
kuona kwamba serikali ya CCM inavyoweza kuvitumia vibaya vyombo vya
dola, kwa utaratibu jinsi ulivyo ili kuruhusu watu waingie katika ukumbi
wa bunge ni lazima kutengua kanuni ili watu waeze kuingia lakini
kutokana na uovyo na ujinga mkubwa wa serikali ya CCM, ambayo
haizingatii sheria na katiba imeweza kuleta askari wengi pamoja na
majeshi kwa ajili ya kukabiliana na upinzani.
“Jambo
kubwa na baya zaidi na la ajabu ni pale ambapo askali waliovaa magwanda
ya polisi na jeshi wakiwa na silaha za moto walivyoweza kuingia katika
ukumbi wa bunge kwa misingi ya kutaka kukabiliana na wabunge wa
upinzani.
“Jambo
hapa ni kwamba hata wao wanajua kuwa Dk. Shein siyo rais halali wa
Zanziba lakini kwa ubishi wao wanalazimisha kufanya hivyo na kutokana na
hali hiyo ndiyo maana serikali imekuwa ikitumia vyombo vya dola kwa
ajili ya kuthibiti wabunge wa Upinzania ambao wametumwa na Umma wasitoe
mawazo yao,” amesema Lissu.
Mbali na hilo alisema pamoja na kuwa walizuiliwa
kuendelea na bunge, kwa ajili ya kuwasilisha hoja zao kwa watanzania
lakini watatumia mbinu nyingi za kufikisha ujumbe kwa jamii kwani kwa
sasa kuna kila mikakati ya kuhakikisha wanataka kuuzima upinzani.
Akizungumzia kuhusu kanuni za bunge kwa sasa alisema
kama ilivyo katiba ya sasa ilivyo na makosa kibao ndivyo na kanuni za
bunge zinavyotakiwa kurekebishwa kwani kuna makosa mengi zaidi.
Kwa upande wao wabunge wa Zanzibar walisema
ni dhambi kubwa kwa Dk. Ali Mohamed Shein kuenedelea kung’ang’ania
kukaa madarakani wakati muda wake umeisha jambo ambalo linaonesha wazi
kuwa ni matumizi mabaya ya madaraka na dola yake.
“Inasikisha
zaidi kuona jinsi Rais wa Zanzibar alivyokuwa siyo muungwana anajua
kabisa kwamba hakushinda uchaguzi, lakini ikumbukwe wakati wa kuvunja
baraza la wawakirishi wabunge wa CCM walimkataa Maalim Seif Shariff
Hamad kama makamu wa kwanza wa rais asiingie katika bunge.
“Lakini
kwa uungwana wa kiongozi huyo aliondoka wala hakuhudhuria kikao hicho
lakini jambo la kushangaza huyu Dk. Shein amekomaa sasa inafikia hatua
anazomewa bila kuwa na aibu sasa huo ni uongozi gani na anamuongoza
nani,” amesema.
“Tunamuuliza Rais Magufuli, ni nani akapeleka vifaru na kuongeza askari wengi katika nchi za Zanzibar na ni kwa sababu gani.
“Kwa
sasa hali ya Zanzibar si shwali kwani kila jambo sasa limelala kwani
hata watalii hawaji kama ilivyokuwa mwanzo, mbali na hilo kuna hali ya
sitofahamu ni kwani nguvu nyingi ya vyombo vya dola inaelekezwa
Zanzibar,” alisema mmoja wa wabunge wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment