Dondoo Muhimu za Hotuba Ya Rais Magufului Jana Bungeni - LEKULE

Breaking

21 Nov 2015

Dondoo Muhimu za Hotuba Ya Rais Magufului Jana Bungeni

=====>>Dondoo  Muhimu  za  Hotuba  Ya  Rais  Magufului  Jana  Bungeni <<=====

 *********
Rais Magufuli mchana huu   analizindua  rasmi  Bunge  la  11  la  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania  mjini Dodoma ambapo pia atatoa mwelekeo wa Serikali yake ya Awamu ya Tano katika miaka mitano ijayo.

Kabla  ya  kuingia  ndani  ya  ukumbi  wa  Bunge,  Rais  amekagua  gwaride  maalumu  lililoandaliwa  kwa  ajili

Awali, kabla  ya  Rais  Magufuli  kuingia  Bungeni,Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alitoa hoja ya kutengua kanuni ili kuwaruhusu viongozi wa kitaifa kuingia bungeni kushuhudia Rais Magufuli akihutubia Bunge.

Tundu Lissu: Napenda tupate muongozo kuhusu baadhi ya wageni kuwakaribisha ndani, kwa hali ilivyo leo hatuna Rais wa Zanzibar, hatuna makamu wa kwanza au wa pili halali wa Zanzibar, hatuna spika wala baraza la wawakilishi Zanzibar.

Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar muda wa serikali ya Zanzibar uliisha tangu Novemba 2.

Naibu spika amemjibu kwa kusema kifungu pia kinasema Rais wa Zanzibar anafikia ukomo mpaka Rais mpya anapoapishwa.

Update
Muda  huu  Rais  wa  Zanzibar  ndo  anaingia  Bungeni,lakini  kuna  hali  ya  vurugu. Wabunge  wa  Ukawa  wanazomea  huku  wakisema  Maalim Seif...... Maalim Seif........Maalim Seif.......Maalim Seif

--> Wabunge  wa  CCM  nao  wanashangilia  huku  wakisema  CCM......CCM....CCM

Update:
Wabunge  wa  UKAWA  Watolewa  Nje  ya  ukumbi  wa  Bunge

Updates:
Rais Magufuli  ameanza  kuhutubia  bunge

-Anasisitiza  kutimiza  ahadi zake  alizoahidi
-Analipongeza jeshi  la  polisi  na  Tume  ya  Uchaguzi  kwa  kufanikisha  zoezi  zima  la  uchaguzi

-Kampongeza  sana  Zitto  Kabwe  kwa  kutozomea  na  kutoka  nje  kama  walivyofanya  wabunge  wengine  wa  upinzani

-Rais  Magufuli  anawapongeza  marais  wastaafu  waliomtangulia  kwa  nzuri  walizofanya

-Kasema  tumemaliza  uchaguzi  tukiwa  wamoja, hivyo  serikali  yake  itahakikisha  inadumisha  amani  hii  kwa  gharama  yoyote

-Rais  amesema  wakati  wa  kampeni, wananchi  walitoa  malalamiko mengi  kama Rushwa,migogoro  ya  ardhi,kuhodhi  maeneo bila kuendelezwa,uvivu, matumizi mabaya ya mali za umma, matatizo  ya  maji 

-Kasema  eneo  lingine  lililolalamikiwa  ni  Uwepo  wa  Rushwa  TRA na  ukwepaji kodi, Tanesco  kukata  umeme hovyo, watumishi wa maliasili kujihusisha  na  ujangili

-Mengine  yaliyolalamika  ni  ubovu  wa  huduma  za  afya, lugha chafu za waaguzi na tozo za ajabu

==>Mh.Spika nimeamua kuyataja haya  ili tujue pakuanzia

-Sehemu nyingine  inayolalamikwa ni uhamiaji, pia  suala  la  Elimu ambapo kuna malalamiko ya walimu na huduma mbovu kwa wanafunzi
 
-Lawama  pia  zilitolewa katika sekta ya  madini ambapo wazawa  hawanufaiki,Mizani rushwa imekithiri,Mahakamani haki zinapindishwa, uvuvib haramu, wakulima kutopewa pembejeo za kilimo

-Eneo lingine ni uchakavu wa Reli, kuzorota kwa shirika la ndege

==> Hizi  ni  baadhi  ya  kero  ambazo  nimezitaja  ili  kwa pamoja tusaidiane  kuzitafutia  ufumbuzi

Pamoja  na  kero  hizo, kuna mambo mengine ambayo tumejipanga kuyasimamia na  kuyatatua. Mambo  hayo  ni;

1. Kuulinda  muungano wetu 
2. Kuimarisha mihimili ya Serikali 
-Tutahakikisha  kuwa mihimili yetu ya Bunge na Mahakama  inapata pesa za kutosha ili iweze kufanya kazi zake kwa uhuru

3. Mchakato wa katiba mpya.
-Serikali yangu inatambua kazi kubwa iliyofanywa na watangulizi wetu pamoja na bunge la katiba lililotupatia katiba pendekezwa.Tunaahidi  kutimiza wajibu wetu kumalizia kiporo hiki tulichoachiwa

4.Uchumi na matarajio ya wananchi
  -Tutaboresha miundo mbinu  ili kuinua uchumi. Tumejipanga kuzijenga upya Reli zetu ili  kuboost vizuri uchumi wetu
-Tuna gesi na madini,tutahakikisha wananchi wote wananufaika na rasrimali hizi.

5.Ujenzi wa Viwanda
-Serikali ya awamu ya tano itaweka kipaumbele katika ujenzi wa viwanda
 -Tutaanza  na  Viwanda Vilivyopo  na  kuhakikisha vinafanya kazi
 -Waliobinafisishwa viwanda hivyo  nawataka  waanze  kazi  mara moja.Wakishindwa tutawanyang'anya.
- Tumejipanga kuhimiza  na  kushawishi  wawekezaji  kuwekeza  zaidi  nchini ili  kukuza  zaidi uchumi  wetu

Sura  Ya  Viwanda  Tunavyotaka  Kuviunda
-Sura  Ya  Kwanza: Ni vile ambavyo malighafi  yake  itatoka  ndani  ya  nchi
 
-Sura  Ya  Pili  ya  Viwanda hivi  ni  vile  vya  kuzalisha  vifaa  ambavyo  vitatumiwa  zaidi  ndani  ya  nchi

***Viwanda hivi  vitakuwa  na uhakika wa soko ndani  ya  nchi  

-Sura  Ya  Tatu  ya  Viwanda  hivi  ni  kuzalisha  ajira  nyingi  kwa  watanzania

6. Kilimo, Mifugo  na  Uvuvi
-Tutaziangalia  sekta  hizi  kwa  mtazamo  wa  kibiashara  ili  kukuza  viwanda  vyetu.

-Tutahakikisha wavuvi hawavamiwi na majambazi
-Tutafuta kodi za wakulima ambazo hazina ulazima
-Wanachi hawatanyang'anywa ardhi zao kiubabe 

7.Umasiki na Ajira
-Nakiri,pengo la wenye nacho na wasio nacho linazidi kuwa kubwa.
-Tumejipanga kupunguza umasikini  na  kukuza ajira kwa kutilia  mkazo uanzishwaji  wa  viwanda, uvuvi, mifugo  na  kilimo  kama  nilivyosema
-Tumejipanga pia  kuwawezesha  vijana  kwa  kuwaandaa  kielimu na  kiujuzi 
-Tutahakikisha vyuo vyetu vinawaandaa vijana kiufundi
-Tutawapa vijana mitaji ya kuanzisha makampuni kulingana na fani zao
-Vijana wataanzisha saccoss zao na watatakiwa kujiunga na mifuko ya jamii   

==> Makundi maalumu ya Bodaboda,mamalishe na Machinga
- Ushuru  usio wa lazima kwa machinga, mama lishe tutaufuta
-Nawataka viongozi wote wa halimashauri  wasiwanyanyase  watu  hawa  kwa  namna  yoyote  ile  na  sitawavumila.

8. Afya  
-Tutaimarisha huduma za afya pale zilipo  na  kuzianzisha pale  ambapo  hazipo
-Tutawapatia mafunzo watumishi wake ndani na nchi
-Tutawapatia vifaa vya kutosha ili kuondoa ulazima wa watu kutibiwa nje
-Tutaongeza bajeti ya wiraza ya afya.

9. Elimu
-Tutaongeza mkazo katika masomo ya sayansi
-Tutahakikisha vifaa  na  maabara vinaongezwa
-Kuanzia Mwakani elimu ya shule  ya  msingi  hadi  kidato  cha  nne  ni  Bure na hakutakuwa na michango.
-Wanafunzi  wa  Vyuo  watapata mikopo kwa wakati
-Matatizo  ya  walimu yatatiliwa  mkazo

10. Maji
-Tutaongeza upatikanaji wa maji kwa asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini.
 -Hatutaki akina mama kubeba ndoo kichwani.Tutaboresha miundo mbinu  ya maji

11.Umeme    
-Tutakamilisha  miradi  iliyopo na mingine mipya itajengwa ili kuhakikisha upatikanaji wa umeme kwa kiwango kikubwa.
-Pale mtera kuna hujuma, watu wanafungulia maji ili yamwagike hovyo  wauze  mafuta. Naahidi kupambana Nao.

12.Madawa ya Kulevya.
-Tunaahidi  kuusaka  kwa gharama zozote mtandao wa wauza madawa ya kulevyo.
-Tutashughulika na wakubwa sio vidagaa  na  hatutawaogopa  na  mungu  anisaidie

13. Rushwa  na  Ufisadi.
-Nachukia sana Rushwa na ufisadi 
-CCM tumejengwa katika imani ya kukataa  Rushwa na Ufisadi, japo sina  imani sana kama wanachama wa  sasa hawatoi na kupokea rushwa.
-Wananchi wamechoka sana na Rushwa na hawako tayari kuvumilia UPUUZI  wa  serikali  kuwavumilia mafisadi  na  wala  Rushwa
-Dawa  ya  jipu  ni  KULITUMBUA......Nimejipa  hii kazi  ya  kuyatumbua  haya  majipu
-Nafahamu ugumu wa vita  niliyoamua  kupambana nayo  maana  Rushwa  hutendwa  na  viongozi  wakubwa  wa  nchi, lakini naamini  wananchi  wataniunga  mkono  katika  mapambano  haya  ya  Rushwa  na  Ufisadi.
-Ili  kulitatua  tatizo  hili, nimedhamiria  kuanzisha  mahakama  ya  Rushwa  na  Mafisadi
- Kiongozi  yeyote  ntakaye  mteua  na  kujihusisha  na  Rushwa  NITAMTIMUA  MARA  MOJA  na  hatua  nyingine  za  kisheria  zitachukuliwa  

14. Baraza dogo la Mawaziri
-Nimejipanga kuunda serikali ndogo itakayojikta kuwatumika  wananchi.
-Watumishi  wavivu, wazembe  hawatakuwa  na  nafasi  ndani  ya  serikali  yangu
-Tumewavumilia  vya  kutosha.....Sasa  Inatosha, hatutawafumbia  macho
-Pamoja  na  hilo, lakini  pia  tumejipanga  kupunguza  kodi  ya  wafanyakazi  na  kuboresha  mishahara  yao.
 
15.Ukusanyaji wa Mapato na kubana matumizi
-Tumejipanga  kushughulika  na  wakwepa kodi  wote ili  kukuza  uchumi wetu  
-Safari zote za nje  ya nchi tutazifuta  na  tumeshaanza.
-Hata  kama  ikitokea  kiongozi  akasafiri  hatutaruhusu  aambatane  na  msafara  mkubwa  usio  na  ulazima.
-Kuna watu hapa wameshasafiri nje ya nchi mara nyingi zaidi kuliko walivyosafiri kwenda kwa wazazi wao
-Takwimu  nilizonazo  ni  kuwa  kwa  mwaka  huu  wa  pesa  zaidi  ya  bilioni  356.324  zilitumika  kwa  safari  za  nje.Huu  ni  ubadhilifu  wa  mali  za  umma
-Warsha,semina  na  makongamano  yote  tutayafuta 
-Sheria  ya  manunuzi  nayo  ni  mdudu  mbaya. kalamu  ya  1000  hununuliwa  kwa  sh.10,000. Sheria  hii  lazima  tuibadilishe 
-Magari  ya  gharama  kwa viongozi  waandamizi  wa  serikali  yatadhibitiwa 

 ****Vipaumbele  Vya  Serikali  Yangu
1.Kupunguza  urasmu
2.Kubana matumizi
3.Kurejesha nidham ya serikali na utumishi wa serikali
4.Kupunguza ukubwa wa baraza la serikali
5.Tutaongeza  nidham ya matumi serikalini

==>  Rais  Magufuli amehitimisha  Hotuba  yake na  kutangaza  kulifungua  Rasmi  Bunge  la  11

-Baada  ya  Rais  Magufuli  kumaliza  Hotuba  yake, Waziri  mkuu ameitwa  kwa  ajili  ya  kutoa  hoja  ya  kuahirisha  kikao  cha  kwanza  cha  bunge  la 11

-Waziri  Mkuu  ametoa hoja ya kuliahirisha  Bunge  hili la 11 hadi  tarehe 26 Jaruary 2016 

No comments: