Ndugu zangu,
Duniani
hapa hakuna shule ya kujifunza uungwana. Watanzania leo tumeshuhudia
jambo la aibu kubwa kwa taifa na mbele ya wageni kutoka nje wakiwamo
mabalozi. Ni pale UKAWA walipoamua kumfanyia fujo Dr Ali Mohammed Shein,
Rais wa Zanzibar alipokuwa akiingia Bungeni.
Kwangu tafsiri ya kwanza kwa kilichokuwa kikifanywa na UKAWA mle ukumbini ni wabunge wale wa UKAWA kukosa uongozi wenye kutanguliza hekima na busara. Mwenye kutanguliza hekima na busara, na kwa kuzingatia mila na desturi zetu za Kiafrika, jambo lile si la kuwaelekeza wafuasi wako kulifanya.

Na
kilichoonekana pia ni ukweli kuwa ndani ya UKAWA ni wachache wenye nguvu
hata za kuamrisha ambapo wengine hawawezi kupinga. Naamini si wote
waliokuwa wakizomea walifurahia walichokuwa wakifanya, bali, walitaka
kuwaonyesha waliowatuma kuwa wanafanya, maana, walionekana. Ni sasa,
ndani ya UKAWA linaonekana pengo la viongozi wenye hekima na busara aina
ya Dr Slaa na Profesa Lipumba.
Naamini
kabisa, mbele ya Watanzania walio wengi, hakuna mavuno waliyoyapata
UKAWA kwa kitendo kile walichomfanyia Dr Shein, bali hasara kubwa ya
kisiasa. Kwa kitendo kile UKAWA wamejidhohofisha na wakati huo huo
kuwaimarisha CCM.
Si ajabu,
John Magufuli aliamua kushindilia msumari mwishoni mwa hotuba yake kwa
kumwambia Spika awavumilie wapinzani na waendelee kuwafundisha. Akiwa na
maana bado hawajakomaa.
Na kwa
vile mtazamo huo wa Magufuli yumkini ndio unaofanana na wananchi wengi
mitaani na vijijini, basi, hiyo ndio hasara ya kisiasa ninayoisema.
UKAWA wana nafasi ya kujirekebisha, na waanze kwa kumwomba radhi Dr
Shein na kuwaomba radhi Watanzania.
No comments:
Post a Comment