Chama
Cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar, kimedai kuwa na ushahidi mzito,
kuhusu namna Uchaguzi Mkuu ulivyoharibiwa kabla ya Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (Zec) kufuta matokeo ya uchaguzi huo.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM (Zanzibar), Waride Bakar Jabu,
alipozungumzia mgogoro wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar jana, akidai
wamekusanya taarifa na ushahidi wa kutosha kuhusu mbinu zilizofanyika
kuharibu uchaguzi na kusababisha hasara kwa serikali.
Waride
alitahadharisdha kwamba, iwapo Zec itaendelea kusuasua kuanika uhalisia
wa uchaguzi ulivyofanyika, CCM itaingilia kati kwa kuweka mambo
hadharani ili wananchi wafahamu ukweli wake.
“CCM tuna ushahidi wa kutosha jinsi uchaguzi ulivyovurugwa na wapizani wetu, lakini Mungu hakuwa pamoja na wao,” alisema Msemaji huyo wa CCM Zanzibar.
Aidha, Waride alisema kuwa kimsingi CCM inaunga mkono uamuzi wa Zec wa kufuta matokeo na kutangaza kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu.
Alisema
kwamba inasikitisha kuona Zec imeshindwa kutangaza tarehe ya kurudiwa
kwa uchaguzi kwa wakati na kuwapa wakati mgumu wananchi ambao wanahitaji
kufahamu lini watapata haki ya kuchagua viongozi wao akiwamo Rais wa
Zanzibar.
Waride
alisema kuwa wananchi wanatakiwa kutagaziwa tarehe ya kufanyika Uhaguzi
Mkuu mapema ili wapate nafasi ya kujitayarisha na kujipanga kabla ya
kufanyika kwa uchaguzi huo.
Aliongeza
kuwa wananchi wamekuwa wakifuatilia kwa karibu tarehe ya kufanyika kwa
uchaguzi wa marudio bila kupata majibu tangu Zec kufuta matokeo ya
Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu.
Pia
aliongeza kuwa CCM inaendelea kujipanga na uchaguzi wa marudio, pamoja
na kuwashukuru wanachama wake na wananchi walivyojitokeza katika
uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka huu kabla ya matokeo ya uchaguzi huo
kufutwa na Mwenyekiti wa Zec, Jecha Salim Jecha, Visiwani Zanzibar.
Jecha
alitangaza kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu huo kwa madai ya
kubaini makosa tisa yalifanyika kwenye uchaguzi huo, ikiwamo idadi ya
kura kuongezeka kuliko idadi ya wapigakura waliosajiliwa katika Daftari
la Kudumu la Wapigakura katika vituo mbalimbali vya uchaguzi.
No comments:
Post a Comment