Aliyekuwa
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi ambaye sasa ni
Mkuu wa Chaneli ya Maisha Magic Bongo, akiwa katika moja ya shughuli za
Dstv hapa nchini
Aliyekuwa Meneja Uhusiao wa
MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi amepata nafasi ya juu katika
kampuni ya MultiChoice na kuwa Mkuu mpya wa Channeli ya Maisha Magic
Bongo.
Katika taarifa yake kwa
waandishi wa habari iliyotumwa leo, Barbara Kambogi amewashukuru na
kuwapongeza wanahabari wote nchini kwa kushirikiana naye kwa kipindi
chote cha kazi zake hapa nchini huku akihidi kuendelea kudumisha
mahusiano hayo zaidi hata katika nafasi yake hiyo mpya.
“Nashukuru kwa dhati kwa support yenu niliyoipata toka mwanzo hadi sasa. Hii sio kwaheri, bali kwaheri ya kuonana kwasababu cheo hiki bado kinaniwezesha kuwasiliana nanyi, kwa hiyo mara kwa mara mtasikia kutoka kwangu. MultiChoice Tanzania ipo kwenye mchakato wa kupata PR mwengine lakini kwa sasa Meneja Masoko wa DStv, Furaha Samalu atashika nafasi yangu hadi atakapopatikana mwengine” alieleza Barbara Kambogi katika taarifa yake hiyo.
Maisha Magic Bongo yenye makao yake makuu Nairobi, Kenya imekuwa ni miongoni mwa channel zenye mafanikio makubwa kwa kukuza lugha ya kiswahili ikiwemo kurusha filamu za Kitanzania ikiwemo Bongo Movie, Muziki wa Kitanzania na filamu na vipindi vingine vikiwemo vile vilivyotafsiria kiswahili.
Maisha Magic Bongo inakuwa
miongoni mwa channel ya burudani barani Afrika inayoandaliwa na M-Net
huku ikiruka hewani kupitia chaneli 160 ya DStv kila siku
kupitia vifurushi vyote vya Access, Family, Compact, Compact Plus,
Premium na Dstv Bomba.“Nashukuru kwa dhati kwa support yenu niliyoipata toka mwanzo hadi sasa. Hii sio kwaheri, bali kwaheri ya kuonana kwasababu cheo hiki bado kinaniwezesha kuwasiliana nanyi, kwa hiyo mara kwa mara mtasikia kutoka kwangu. MultiChoice Tanzania ipo kwenye mchakato wa kupata PR mwengine lakini kwa sasa Meneja Masoko wa DStv, Furaha Samalu atashika nafasi yangu hadi atakapopatikana mwengine” alieleza Barbara Kambogi katika taarifa yake hiyo.
Maisha Magic Bongo yenye makao yake makuu Nairobi, Kenya imekuwa ni miongoni mwa channel zenye mafanikio makubwa kwa kukuza lugha ya kiswahili ikiwemo kurusha filamu za Kitanzania ikiwemo Bongo Movie, Muziki wa Kitanzania na filamu na vipindi vingine vikiwemo vile vilivyotafsiria kiswahili.
Mataifa jirani ya Afrika
Mashariki ikiwamo Kenya, Uganda, Ethiopia, DRC na mengineo yakiwemo
Nigeria na kwingine wanapata huono huo wa channel hiyo bora kwa sasa ya
kiswahili.
Mkurugenzi M-Net Kanda ya
Afrika Magharibi, Wangi Mba-Uzoukwu (katikati) akiwa kwenye picha ya
pamoja na Movie Stars wa nchini Nigeria, Rita Dominic na Desmond Elliot
mara baada ya mkutano na waandishi wa habari hivi karibuni
Aliyekuwa
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (kulia)
akifurahi jambo Wanahabari Sidi Mgumia (katikati) na Mama Mhina katika
moja ya matukio ya DStv nchini Tanznia. (Picha ya Maktaba yetu).
No comments:
Post a Comment