Mtoto wa miaka 5 apoteza maisha baada ya kubakwa na watu wasiojulikana Mkoani Kigoma! - LEKULE

Breaking

27 Nov 2015

Mtoto wa miaka 5 apoteza maisha baada ya kubakwa na watu wasiojulikana Mkoani Kigoma!


[KIGOMA] Mtoto mmoja alitambulika kwa  majina, Asifiwe Amos mwenye miaka mitano (5) na mkazi wa kijiji cha Katuguru Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma amefariki dunia baada ya kubakwa na watu wasiojulikana na kupelekea kifo chake hicho.
Akizungumza na Waandishi wa habari hii leo, Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma SACP Ferdinand Mtui amebainisha kuwa, tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 9:30 arasili katika kijiji cha Katuguru wakati mtoto huyo akicheza na wenzake.
Kamanda Mtui amebainisha kuwa, wakati watuhumiwa wakifanya kitendo hicho mtoto yule alikuwa akipiga kelele hivyo watuhumiwa wakaamua kumziba pua na mdomo jambo lililopelekea kukosa pumzi na kufariki.
“Katika eneo la tukio kulikuwa ni mita 200 kutoka nyumbani kwao  mpaka mwili ulipokutwa  na inavyoonekana sehemu alipofanyiwa kitendo hicho ni kwenye nyumba yenye uzioa mana kutoka kwenye hiyo nyumba kulikuwa na mibuluzo ya miguu hadi ulipokuwa mwili kitu kinachofanya tuamini kuwa baada ya kumbaka walimbuluza mpaka nje” alisema Kamanda Mtui.
Aidha Kamanda Mtui alisema kuwa,  Jeshi la Polisi linamshikilia mtu mmoja kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo.
Hata hivyo Kamanda Mtui aliwataka wazazi kuwa makini wanapowaacha watoto wao nyumbani kwa kuwaacha chini ya uangalizi wa watu wakubwa ili kuepusha kutokea kwa matukio kama haya.

“Wazazi wa mtoto huyo waliondoka asubuhi kwenda kwenye shughuri zao na kumuacha mtoto akicheza na wenzake lakini hakuna mtoto yule alichukuliwaje na watuhumiwa na hata wale watoto wenzake hawajui chochote, Wazazi walitakiwa kujua wanamuacha mtoto wao katika mazingira gani” aliongeza Kamanda Mtui.

No comments: