Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akitoa hotuba ya
ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Maliasili nchini leo tarehe 26
Novemba 2015 katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii Kampasi ya Bustani Jijini
Dar es Salaam. Mkutano huo umeshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wa
Wizara zenye muelekeo wa Maliasili, Sekta binafsi, NGOs, Waandishi wa
habari na wadau wengine. Mada mbalimbali kutoka katika Sekta ndogo za
Wanyamapori, Misitu, Utalii, Mambo ya Kale na Uvuvi zimewasilishwa.
Baadhi ya Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru wa pili kulia
akiwa kwenye picha ya pamoja na balozi wa Ujerumani hapa nchini Mhe.
Egon Kochanke wa pili kushoto muda mfupi baada ya kufungua Mkutano huo.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Mkambusho ya Taifa Prof. Audax Mabula.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akihojiwa na
Mwandishi wa Habari wa Azam TV, Jamal Hashim muda mfupi baada ya
ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Maliasili nchini uliofanyika
leo tarehe 26 Novemba 2015 katika Ukumbi wa Chuo cha Maliasili Jijiji
Dar es Salaam. Mkutano huo umejadili mambo mbalimbali ikiwemo mafanikio,
changamoto na fursa zinazopatikana katika sekta hiyo muhimu
inayochangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa. Miongoni mwa
changamoto kubwa alizozieleza Katibu Mkuu huyo ni Ujangili na Uharibifu
wa misitu jambo ambalo amesema Serikali na Wizara imejiapanga kupambana
nalo na kuwaomba wadau kushirikiana na Serikali katika vita hiyo.
Baadhi ya wadau walioshiriki Mkutano huo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Mipango na Sera Bi. Mary Faini kutoka Wizara ya Maliasili
na Utalii akiwasilisha mada kuhusu Mafanikio, Changamoto na Fursa
zinazopatikana katika Sekta ya Maliasili nchini Tanzania.
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment