Makamu
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Mh. Idd Ramadhan Mapuri
(katikati) akizindua taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na
Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia
Tanzania. kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu
na Utawala Bora Bi. Mary Massay na (kulia) ni mmoja wa wajumbe
walioshiriki kuandaa ripoti hiyo, kutoka nchini Kenya katika taasisi ya
ACHPR, Dk. Naomi Kipuri.(Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
Jamii
ya watu wa asili na makundi yao wameiomba Serikali ya Tanzania kutambua
uwepo wao hapa nchini ikiwemo kuwatangaza kwa mema na kuwasaidia kwa
misingi ya haki, hutu na kimaendeleo kama watu wengine wanaotambulika
ndani na nje ya mipaka yao.
Hayo
yameelezwa mapema leo jijini hapa wakati wa uzinduzi wa taarifa ya Tume
ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za
watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania wakiwemo makabila ya
Wa-Akiye,Wa- Hadzabe,Wa- IIparakuyio Masai na wengine wengi.
Akielezea
katika uzinduzi huo mmoja wa wajumbe walioandaa taarifa ya Tume hiyo,
ambaye anatoka nchini Kenya, katika taasisi ya African Commission on
Human and Peoples Rights (ACHPR), Dk. Naomi Kipuri amebainisha kuwa
jamii ya watu asilia wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha kutaka kupata
haki zao zao msingi na kutambulika zaidi.
“Utafiti
tuliofanya jamii ya watu asilia wamekuwa katika malalamiko ya muda
mrefu ikiwemo kutaka haki zao za msingi. Ikiwemo masuala ya elimu,
makazi na haki zingine. Pia wameomba Serikali kuwatangaza watu hawa wa
asilia ili wasionekane wageni kwani jamii nyingi bado hazijawatambua na
hata kupelekea kuwavunjia hutu wao” alieleza Dk. Naomi.
Aidha,
Dk. Naomi katika uwakilishi wake wa mada kwenye mkutano huo amelezea
namna ya jamii inavyoendelea kuwaona watu hao ni tofauti kiasi cha
kupelekea watu hao kudumaa na maisha yale yale ya asilia.
Mtangazaji
wa radio Deutsche Welle (DW) ya Ujerumani, George Njogopa akifanya
mahojiano na Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Bi. Mary Massay. Kushoto ni Mratibu wa NGONET Ngorongoro, Samweli
Nangiria.
“Jamii
zingine zinawatenga watu wa jamii ya Wamasai, tumeshuhudia lugha na
matamshi kwenye mizunguko ya watu ikiwemo kwenye madaladala, mitaani
huku wakimuona Mmasai kama mtu tofauti, sasa katika ripoti hii imeweza
kuelezea mambo mengi sana. Ikiwemo suala la Haki ya kuishi, kufanya kazi
na mambo yote kama watu wengine” alimalizia Dk. Naomi.
Kwa
upande wake Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Mh. Idd
Ramadhan Mapuri ameeleza kuwa kupitia ofisi yake itahakikisha
inashughulikia suala hilo la kuwa karibu na watu asilia na kutambua
misingi ya haki zao ambapo amebainisha watu hao wa asilia kwa Tanzania
wanafikia makundi zaidi ya sita.
Kwa
upande wao baadhi ya wawakilishi wa watu hao wa watu asilia wakielezea
katika mkutano huo, waliomba na wao na wapate wawakilishi maalum ikiwemo
Bungeni ama sehemu za maamuzi ikiwemo Halmashauri na maeneo mengine ya
Serikali ilikutambua michakato ya Kimaendeleo kwa kina. “Jambo la ardhi,
ndilo linalotuumiza kwa sasa.
Sie
tunaporwa ardhi yetu kila siku na kesi nyingi ni za kuporwa ardhi na
migogoro ya wakulima na wafugaji, ndani ya migogoro hii ina siri kubwa
bila kujua kiini chake ni wakati wa kufika kule na kupata ukweli zaidi”
alielezea Adam Ole Mwarabu Kwa upande wake, Mratibu wa NGONET
Ngorongoro, Samweli Nangiria ambaye anawakilisha watu hao asilia
anaeleza kuwa, wao wamekuwa wakitambuana kwa desturi ikiwemo suala la
ufugaji na maisha mengine, Jamii nyingine imekuwa wakiwaona wao ni watu
wa tofauti kiasi cha kupora mali zao ikiwemo ardhi, mifugo na mambo
mengine ya msingi.
Baadhi
ya wawakilishi wa Jamii za watu asilia wakiwemo Wahadzabe, Masai,
Wabarabaig na wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora na wadau wengineo wakiwa kwenye picha ya
pamoja wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo juu ya usawa na kutambulika
kama jamii asilia yenye tamaduni na desturi zake.
“Sie
watu asilia tuna mahusiano mbalimbali na jamii zetu za kifugaji licha
ya jamii zingine kutuingilia kwenye maeneo yetu na kupora ardhi yetu.
Watu asilia tunahitajika kutambulika zaidi na hata kupatiwa huduma
muhimu ikiwemo kujengewa shule, vyuo na mahitaji mengine ikiwemo haki na
hutu kama watu wengine.” Alieleza Samweli Nangiria.
Kwa
upande wake, .. ameweza kuipongeza tume ya Haki za Binadamu kwa kuweza
kushughulikia suala hilo na hata kuandaa tukio hilo kwa kushirikisha
wadau wengine wakiemo wao wa asilia.
“Tanzania
ndio nchi ya kwanza kuaandaa kikao cha Afrika kwa watu hawa wa makundi
maalum wa asilia, kilichofanyika mwaka uliopita. Hili ni jambo bora sana
kwani watu asilia tunaendelea kutambulika zaidi.
Ripoti
hiyo iliyozinduliwa ya taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na
Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia
Tanzania, imeweza kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo suala la haki ya
kuishi, Utawala bora na namna ya jamii hizo zinapotokea katika maeneo
yao hapa nchini.
Wadau
wa haki za binadamu wakiwa katika picha ya pamoja katika mkutano huo
baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo ya kuwatambua watu wa makundi asilia.
Mkutano unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Blue Pearl Ubungo
jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa washiriki wa mkutano huo Mhifadhi Mkuu, kutoka ofisi ya Makamu wa
Rais, Bw. Seleman Kisimbo akichangia mada juu ya hali iliyopo sasa
ikiwemo jamii hiyo ya watu asilia na changamoto za Mabadiliko ya tabia
nchi ikiwemo suala la ukame inayowakabili katika maisha yao ya vijijini.
Dk.
Naomi Kipuri wa taasisi ya ACHPR, ya nchini Kenya akijadiliana jambo na
Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Tumaini-Makumira, Bw. Elifuraha
Laltaika.
Baadhi
ya wawakilishi wa Jamii za watu asilia wakiwemo Wahadzabe, Masai,
Wabarabaig na wengineo wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye mkutano huo.
No comments:
Post a Comment