KAMPUNI
ya Freconic Ideaz, imeandaa tamasha la burudani la ‘Instagram party’
litakalofanyika kesho kutwa kwenye Ukumbi wa Escape One Mikocheni jijini
Dar es Salaam likiwa na lengo la kuwakumbusha wapenzi wa muziki,
mavazi na misemo ya kizamani.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba alisema
pia tamasha hilo litahusisha watu wenye ushawishi mkubwa katika mitandao
ya kijamii na wasanii mbalimbali wa muziki na filamu wanamichezo na
wanasiasa na kuweza kufanikisha mashabiki wao kuweza kupiga nao picha
katika red carpert.
Alisema
wadau na marafiki mbalimbali wanaotumia mitandao ya kijamii watakutana
siku hiyo kuweza kufahamiana na kubadilishana mawazo huku wakipata
burudani mbalimbali.
“Kiingilio
katika tamasha hili kitakuwa ni sh. 50,000 kwa viti maalumu na vile vya
kawaida ni sh. 10,000, ambapo halitaishia hapa ila litaendelea katika
Mikoa ya Mwanza, Morogoro, Tanga, Dodoma na Iringa,” alisema Ngimba.
Alitoa
mwito kwa wadau wa muziki wa mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi
kushuhudia burudani itakayotolewa siku hiyo kwani kuna maboresho makubwa
yamefanyika katika kuongeza ubunifu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Freconic ideaz, Fred Ngimba akifafanua jambo alipokuwa
anaongea na waandishi wa habari jana katika fukwe za Escape One kuhusu
kukamilika kwa maandalizi ya tamasha kubwa la burudani litakalofanyika
jumamosi hii tarehe 28 ,kulia kwake ni Meneja mawasaliano wa Freconic
ideaz Krantz Mwantepele.
Mmoja
wa wadau akitembelea ukurasa wa INSTAGRAM PART TZ kupata taarifa
mbalimbali kuhusu tamasha hili litakalowakumbusha wapenzi wa burudani
nyimbo za zamani ,misemo ya zamani hata mavazi ya zamani kukiwa na kauli
mbiu ya BONGO THROW BACK.
Mkurugenzi
wa Freconic ideaz, Fred Ngimba (kushoto), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu tamasha kubwa la
burudani la Instagram Party litakalofanyika Jumamosi katika viwanja vya
Escape One Mikocheni likiwa na kauli mbiu Bongo Throw Back. Kulia ni
Meneja Mawasiliano, Krantz Mwantepele.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
No comments:
Post a Comment