Mteja wa muda mrefu wa bemki ya Amana Bw Masoud Khalfan (katikati)
akizindua wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Main la benki ya
Amana jijini Dar ka kukata utepe. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa benki
hiyo Dk Muhsin Masoud, Kulia ni mkuu wa idara ya masoko Bw Dassu Mohamed
Mussa, kushoto ni mteja wa siku nyingi wa benki hiyo Bw Dossa.
Mkuu wa idara ya masoko Bw Dassu Mussa kushoto akiwa na mkuu wa
kitengo cha fedha Bw Fahad Hamid siku ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa
wateja.
Benki ya kwanza ya kiislamu Tanzania, Amana Bank imeadhimisha
miaka minne tangu kuanza rasmi kutoa huduma zake kwa wateja mnamo 24
Novemba 2011. Wakuu wa idara Mameneja na wafanyakazi siku ya jumatatu
wote walikutana na wateja na kuwapatia huduma mbalimbali kupitia matawi
yetu yote ya Dar es salaam, Arusha na Mwanza.
Meneja wa tawi la Main Bi Aisha Awadh akimwelekeza kitu mteja wa benki mama Sangawe.
Amana Bank ambayo kwa sasa ina wateja zaidi ya 20,000 na matawi 7
Tanzania nzima, inachukua fursa katika maadhimisho haya kuwashukuru
wateja wake wote kwa kuwa wazalendo na kuichagua Amana Bank kama
pendekezo lao kwa huduma za kibenki. Amana Bank inaahidi kuendelea
kuwekeza na kukuza mtandao wake na kuleta bidhaa na huduma bora Zaidi na
za kisasa. Amana Bank mpaka sasa ina matawi saba ambapo manne yapo
jijini Dar nayo ni Tandamti, Lumumba, Nyerere na main ambapo ndipo makao
makuu ya benki hiyo ya aina yake nchini.
Mfanyakazi wa benki ya Amana (Kushoto) akiwahudumia wateja kwa viburudisho katika siku ya wiki ya huduma kwa wateja wiki hii.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Amana wakipata picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dr. Muhsin Salim Masoud
amesema, “Katika kipindi hiki maalum kwa benki yetu, tutashirikiana na
wateja wetu wa ndani na wa nje kwa kuwapatia huduma bora zaidi.
Tunaamini wateja wetu ndio muhimili wa mafanikio yetu, lengo letu kubwa
ni kuwaridhisha wao hivyo tumejidhatiti kuwapa huduma bora muda wote
bila kujali mahali walipo. Tunawaahidi wateja wetu huduma za kiwango
cha juu kwa ajili ya mahitaji yao ya binafsi au kibiashara muda wote.
Mtoa huduma kwa wateja Bi Zainab wa tawi la Mwanza akimhudumia kwa viburudisho mteja wa benki hiyo.
Mteja huyu akijipatia huduma katika tawi la Mwanza
Huduma kwa wateja.
Maadhimisho haya yatahitimishwa ijumaa ya 27/11/2015, kwa hafla ya
kuwazawadia wateja na wafanyakazi katika matawi ya Amana Bank ambapo
mkurugenzi wa benki hiyo Dk Muhsin Masoud atakuwa katika tawi la jijini
Mwanza mjini kukutana na wateja na kupokea maoni na ushauri wa kila
aina utakaotolewa na wateja wao.
Baadhi ya wateja wakijipatia huduma katika benki ya Amana tawi la jijni Arusha.
Huduma kwa wateja zikiendelea jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment