Nawasalimuni
nyote katika jina la nchi yetu nzuri Tanzania,
Jina ambalo huko nyuma sote tuliliimba “Tazama ramani utaona nchi nzuri,
yenye mito na mabonde mengi ya nafaka…nchi hiyo mashuhuri huitwa
Tanzaniaaa!”
Hakika wimbo huu vijana wengi siku hizi wanashindwa kuuimba, kwa nini?
Uzuri wa taifa lao haupo tena, umepotezwa na baadhi yenu watumishi wa
umma
wasio na uadilifu.
Sio
siri vijana wetu kwa muda mrefu wameshindwa kujivunia taifa lao,
wameshindwa kuongea mbele za watu kwa sauti kubwa kwamba wao ni
Watanzania,
uzuri wa taifa lao na sifa nzuri ya nchi yao imeharibiwa na vitendo kama
ufisadi uliokithiri ambao umesababisha wachache katika taifa kunufaika
huku wengi
wakiteseka.
Ndugu
zangu watumishi wa umma,
Ni kwa kupitia jina la nchi hii ndiyo leo nawaandikieni, kuwakumbusha
juu ya wajibu wenu ambao kwa muda mrefu sana umekuwa hautimizwi
ipasavyo!
Kwanza kabisa niseme wazi kwamba nayafahamu mateso yenu, nayafahamu
mahangaiko yenu ya maisha magumu, ambayo wakati mwingine yamefanya
uaminifu wenu kutikiswa.
Pamoja na hayo yote nasema hakuna jambo hata moja linalohalalisha kwenu
ninyi kupoteza vigezo vitano muhimu vya utumishi wa umma ambavyo ni;
1.UADILIFU
2.UAMINIFU
3.KUSEMA KWELI DAIMA
4.UZALENDO NA DHAMIRA
5.HOFU YA MUNGU.
Yeyote
kati yenu aliyehalalisha kuondoka kwa vitu vitano nilivyovitaja hapo
juu kwa sababu ya aidha kipato kidogo anachokipata serikalini,
akavunjika moyo na
kuacha kuwatumikia wananchi, ama akachagua kuendeleza rushwa na kukosa
uzalendo, huyu hatufai kuwa mtumishi wa umma.
Kwa
muda mrefu mmekuwa
mkilalamikiwa, mkinung’unikiwa na wananchi kwa sababu ya utendaji mbovu
unaosababishwa na kukosekana kwa mambo matano niliyoyataja hapo juu,
kwa kweli ilionekana kana kwamba uadilifu katika taifa hili hauwezekani
tena, vivyo hivyo uaminifu, kusema kweli, uzalendo na hofu ya Mungu
vilitoweka.
Uchaguzi
uliofanyika Oktoba 25, 2015 na kumwingiza madarakani rais ambaye hawezi
kumaliza hotuba yake bila kusema “TUNAMTANGULIZA MUNGU
MBELE” Dk. John Pombe Joseph Magufuli umerejesha tena imani ya
Watanzania kwamba, kumbe utumishi wa umma uliotukuka unawezekana, yote
haya
yamefanyika ndani ya siku chini ya arobaini tangu aingie madarakani!
Kwa
matendo yake hayo, nimesikia kwa masikio yangu watu waliompinga Rais
Dk. Magufuli wakati wa kampeni wakijuta na kusema: “Laiti ningejua
ningempa kura yangu!” haya yanatokea ndani ya siku chini ya hamsini
tangu rais huyu aingie madarakani, upepo umebadilika, utumishi wa umma
uliowekwa
madarakani na watu kwa ajili ya watu kumbe unawezekana.
Ule
msemo wa wazungu usemao “Once you shake the top, you have shaken the
bottom” yaani
ukishatikisa juu, tayari utakuwa umetikisa na chini, sasa umedhihirika
kwamba ni kweli. Tanzania inakimbia mbio, kuanzia serikalini mpaka
kwenye sekta
binafsi, adui uvivu ameanza kupotea kwa sababu tu raia aliyeingia
madarakani sio mvivu.
Kwa mara ya kwanza maishani mwangu nimeanza kusikiliza taarifa za habari
na kusikia habari za kamatakamata, fukuzafukuza, kila kona ya nchi.
kila
kiongozi,
kila mtendaji sasa anajaribu kutimiza wajibu wake, yote haya kwa sababu
amebadilishwa mtu mmoja tu juu ambaye kauli mbio yake ni “HAPA KAZI
TU!”
Ndugu zangu Watumishi wa Umma,
Nawaandikieni barua hii kuwakumbusha kwamba ile kauli yenu ya kusema
“huu ni moto wa mabua” naomba muiache, anayesema hivyo hamfahamu vizuri
rais wetu, kwa wanaomfahamu hawawezi hata siku moja kutoa kauli hiyo,
haigizi, haya ndiyo maisha yake, ni kama mapafu ambavyo kazi yake ni
kupumua,
ndiyo ilivyo kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Ndugu
zangu,
Nawasihi mfanye kazi, timizeni wajibu wenu mliopangiwa kwa faida ya
taifa hili, ambaye hatayasikia maneno haya, hakika ajiandae kukumbuka
ninachokisema
kwani mfumo utamtema! Ni wakati wa kuchapa kazi, si wa kuchati kwenye
mitandao ya jamii saa ya kazi.
Tukifanya
jambo hili kwa pamoja, ninawahakikishieni
taifa letu litasonga mbele kutoka hapa tulipo kwenda tunakotakiwa
kwenda, rais wetu ni MUADILIFU, ndivyo itakavyokuwa kwa Makamu wake wa
Rais Samia
Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, serikali nzima na
hatimaye vijijini, vivyo hivyo katika uchapakazi, kama rais wetu si
mvivu, wavivu
wote watang’oka, watake wasitake.
Matarajio
yangu ni kwamba kama watumishi wa umma mtatimiza vyema wajibu wenu,
mtafanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo wa hali ya juu,
lazima kipato cha taifa letu kitaongezeka na maisha yenu yataboreshwa na
rais huyu huyu tuliyemweka madarakani.
Lakini
niwasihi msipoteze hali yenu
ya kujiamini kwa kusema “Rais ni mkali mno” matokeo yake mkawa ni watu
wa kutekeleza mambo kwa nidhamu ya woga, taifa la watu wenye aina hii ya
nidhamu, ambao hutekeleza mambo yao kwa kutaka tu kumfurahisha mkuu huwa
halisongi mbele, matokeo yake huzaa hata uonevu kwa sababu tu mtu
alikuwa anataka aonekane anafanya kazi.
Sidhani
rais wetu ni mtu wa aina hii, bali ni mtu anayependa kufanya kazi na
watu wanaojiamini na wachapakazi na atakuwa tayari kujenga jamii ya watu
wenye
kujiamini si wanaotetemeka ovyo kila wanapokutana naye wakimpa ushauri
anaopenda kuusikia, si ule anaotakiwa kuusikia hata kama
hautamfurahisha.
Nimeyasema
haya kwa sababu msipokuwa makini wale mlioko madarakani, wakuu wa
mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi nk. Mtajikuta mkionea watu au
kuwatoa watu sadaka kwa sababu tu mnataka kumfurahisha mkuu au muonekane
mnafanya kazi na baadaye kupanda vyeo kwa gharama za maisha ya watu
wengine.
Sitaki
kusema mengi siku ya leo, kwa haya machache niliyoyasema nawatakieni
utendaji mwema wa kazi katika Awamu hii ya tano ya HAPA KAZI TU! Tendeni
kazi zenu kwa kujiamini na uadilifu wa hali ya juu, nawahikikisheni
awamu hii ya tano itabadilisha maisha yenu, kama anavyosema mwenyewe
Rais Magufuli,
tumuombee kwa Mungu atimize ndoto yake yakutufikisha kwenye nchi ya
ahadi.
Ahsanteni.
NUKUU
WASALAAM
Eric Shigongo James
No comments:
Post a Comment