Wilayani Bukoba, karatasi za kupigia kura ambazo ziliwekewa alama ya vema kwenye sehemu za wagombea wa udiwani, ubunge na urais, jana ziligundulika nyuma ya bweni la Shule ya Sekondari ya Kahororo.
Karatasi
hizo zilikuwa zimesambaa nyuma ya bweni la wanafunzi wa kidato cha
sita, hali iliyowafanya wanafunzi wahisi kuwapo kwa karatasi zaidi ndani
ya mabweni.
Mmoja wa wanafunzi alisema karatasi hizo zilisambaa nyuma ya bweni hilo baada ya mwanafunzi mmoja kuzirusha kupitia dirishani kutokana na kutuhumiwa kutumiwa na mmoja wa wagombea kwenye jimbo hilo lenye ushindani mkali kati ya Chadema na CCM.

Mmoja
wa walimu, Charles Rushinge alisema aligundua karatasi hizo wakati
akikagua mazingira ya shule na baadaye kutoa taarifa kwa vyombo husika
kwa ajili ya kuchukua hatua.
Hata
hivyo, pamoja na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi
kufika shuleni hapo kushuhudia tukio akiwa na baadhi ya maofisa usalama,
bado hakuwa tayari kutoa ufafanuzi wa idadi ya karatasi za kura na
chanzo cha tukio hilo.
Tukio hilo liliibuka huku yakiwepo malalamiko mengi katika vituo vya Kata ya Kashai kuwa kuna karatasi zimenyofolewa kutoka kwenye baadhi ya vitabu vya kupigia kura, ikiwa ni pamoja na kituo cha Zahanati ya Kashai na Shule ya Msingi na Mafumbo.

Mkurugenzi
wa uchaguzi wa Jimbo la Bukoba Mjini, Aron Kagurumjuri aliwataka
wananchi wapige kura na kudai alipokea vitabu kutoka NEC vikiwa
vimefungwa kwenye maboksi, hivyo tatizo la karatasi hizo za kura si
lake....Tazama Video hiii
No comments:
Post a Comment