Gari la mmoja wa makampeni meneja wa mgombea ubunge Jimbo la Moshi Vijijini kwa tiketi ya CCM, Dk. Cyrill Chami, jana lilishambuliwa na kuharibiwa vibaya na wananchi wakilishuku kuwa na kura bandia.
Katika
tukio hilo lililotokea saa 10:00 alasiri katika kijiji cha Uru Kitandu,
meneja kampeni huyo wa Dk. Chami aitwaye Kizitto George, aliokolewa na
Polisi lakini wakati huo akiwa ameumizwa vibaya kwa kipigo hicho.
Gari
hilo aina ya Toyota Verosa namba T756 CPB liliharibiwa vibaya kwa
kuvunjwa vunjwa vioo, kung'olewa magurudumu yake, kuibiwa redio ya gari
na vifaa mbalimbali kung'ofolewa.
Katibu
wa zamani wa Mbunge Chami, Martin Mallya alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo akisema gari hilo halikuwa limebeba kura yoyote ila
kinachoonekana walikuwa wakimwinda muda mrefu.
"Hivi ninavyoongea na wewe niko hapa Polisi majengo ili kufuatilia nijue amepelekwa hospitali gani ila nimeambiwa gari limeharibiwa vibaya," alisema Mallya ambaye aliwahi kuwa Diwani wa kata ya Okaoni Kibosho kwa tiketi ya CCM.

No comments:
Post a Comment