Tukumbushane: Kinondoni Iliwahi Kuwa Na Mbunge Mzungu..! - LEKULE

Breaking

24 Oct 2015

Tukumbushane: Kinondoni Iliwahi Kuwa Na Mbunge Mzungu..!

Ndugu zangu,
Ni enzi za Mwalimu, aliitwa Derek Bryson, pichani ni wa kwanza kushoto.
Alipata pia kuwa waziri wa kilimo na ushirika. Ni imwasisi wa mpango wa kutenga viwanja Sinza ikiwamo miundo mbinu kama vile mitaa, viwanja vya wazi na maji ya bomba, hata kabla watu hawajajenga.
Derek pia ndiye aliyepelekea Shirika la Posta Na Simy kufungua matawi Kinondoni, Ilala na Temeke.
Alipata kutamka Bungeni; Ni ajabu mtu apande basi na kulipa nauli kutoka Kinondoni aende mjini kununua stempu yenye thamani sawa na nauli yake ya basi, kwanini asingenunulia Kinondoni na kuituma barua yake akiwa Kinondoni?
Na majibu ya Posta na Simu ikawa ni kufungua matawi ya Posta wilayani...! ( Picha hii ni kutoka kwenye kitabu cha Sir Andy Chande, Knight In Africa)

Maggid.

No comments: