Kada wa CCM ARIF Abri kushoto akipiga pushapu
Kamanda wa Uvccm Mkoa wa Iringa Bw Salim Asas akizungumza na wananchi wa jimbo la Iringa Mjini
ARIF akimwombea kura MWAKALEBELA
Kamanda
wa UVCCM Mkoa wa Iringa Salim Asas na Mjumbe wa Mkutano mkuu wa Taifa
CCM Bw Arif Abri wamesema wapo tayari kuleta maendeleo ya jimbo la
Iringa kwa kushirikiana na Frederick Mwakalebela kuwa mbunge wa jimbo la
Iringa mjini
Wakimwombea
kura leo Mwakalebela katika uwanja wa Mwembetogwa wakati wa ufungaji wa
Kampeni za CCM , walisema wapo tayari Kama wafanyabiashara wakubwa
Mjini Iringa kushirikiana na MWAKALEBELA kuleta maendeleo yaliyosimama
kwa miaka mitano.
Asas
alisema inasikitisha kwa kuona wananchi wa jimbo hilo wakitabika kwa
kukosa mitaji wakati jimbo hilo lilikuwa na mbunge na kuna mfuko wa
jimbo ambao ungeweza kusaidia mikopo nafuu.
Hata
hivyo alisema kwa upande wake amekuwa akisumbuliwa na vijana kwa kuomba
kusaidiwa baada ya kukosa msaada toka kwa mbunge wao .
Hivyo
alisema iwapo watampa nafasi ya kuwa mbunge Bw Mwakalebela Wananchi
wategemee maendeleo makubwa zaidi na kwa upande wake atashirikiana na
Mbunge Mwakalebela kuleta maendeleo .
Huku kwa
upande wake Abri alisema akiwa ni mmoja kati ya wadau wakubwa wa
maendeleo jimboni hapo atahakikisha anafanya Kazi ya kuleta maendeleo na
Mwakalebela.
Abri alisema kuwa suala la maendeleo jimboni hapo linahitaji mbunge makini Kama Mwakalebela na si vinginevyo .
No comments:
Post a Comment